Jumamosi, 24 Novemba 2018

Ph.L (FALSAFA YA MAISHA)

FALSAFA YA MAISHA (PHILOSOPHY OF LIFE)
(Ph.L)
Kuna ngazi mbalimbali ambazo mwanafunzi hupanda ili kufikia ngazi ya juu ya elimu anayoitaka na kuna ngazi mbalimbali pia ambazo mwanafunzi wa maisha akazitumia  aidha kupanda au kushuka ili kufikia kilele cha malengo aliyojiwekea.
Kuitwa dereva,mtumishi,mwalimu,askari,mwandishi,mpishi,daktari,mhandisi, au profesa ni majina ambayo huwa na heshima kubwa kwa mtu na kuitwa mfanyabiashara,mjasiriamali,muwekezaji,mwanzilishi,mgunduzi,tajiri,bosi,bilionea ni majina ambayo huwa na heshima pia.

Lakini katika hayo makundi mawili heshima zake zinatofautiana kulingana na zinavyoundwa au kuandaliwa.
Kuna heshima ambayo tayari imeandaliwa ili uvikwe na kuna heshima ambayo utaiunda na kuiandaa wewe mwenyewe heshima hizi zimetofautiana kwa makundi mawili. Kundi la kwanza ni heshima ya nje na kundi la pili ni heshima ya ndani.
Sitaingia kabisa katika kujadili mifumo ya elimu kwasababu inaweza ikawaathiri wadogo zetu ambao bado wapo mashuleni na vyuoni au wale wote waliotoka kuhitimu hivi karibuni.
Chamsingi cha kuwaambia ni waitegemee elimu kama ngao yao na siyo kama mkombozi wao kwasababu kuna vitu viwili uraiani ambavyo havitangamani kabisa yaani vyeti,mtaa na mihangaiko.

SASA TWENDE TUKASOME UPYA NA TUJITUNUKU Ph.L ZETU BILA JOHO WALA VYETI NA HESHIMA TUKAIPATE VILEVILE.
Watu husema hakuna mwalimu mkorofi,mkali na mgumu kumuelewa kama ulimwengu kutokana na njia anayoitumia kufundisha.
Sijajua ulimwengu ni Madam au Sir ila yeye huanza na kukupatia mitihani mfululizo kisha anakuja kukupatia majibu na baadaye usahihi halafu mitihani tena.
Hapa ndipo wengi hushindwa kumuelewa mwalimu huyu alisomea wapi kufundisha namna hii.
Lakini nilichokipenda kutoka kwa mwalimu huyu tangu nimesajiliwa kwenye darasa lake ni namna anavyowatunuku heshima wanafunzi wake pindi wanapohitimu.
Huwa hatoi cheti,tuzo,medali,kombe wala kitu chochote cha kushikika ila anakuvika vazi la hekima,utu na heshima ambalo siyo la kukodishwa ila huwa anakuja kulinyang'anya ikitokea unalitumia vibaya vazi lake na kukurejesha tena kwenye chumba cha mitihani.

MWALIMU HUTOA SHAHADA YA FALSAFA YA MAISHA YAANI (Ph.L) KATIKA KITIVO CHA MAISHA.
Hekima,utu na heshima utakayovikwa huwa inaambatanishwa na shahada ya (Ph.L) yaani falsafa ya maisha. Na sasa twende tukaiangazie shahada hii kiundani ili uipate unahitaji kupitia katika mitihani ipi.

1.MTIHANI WA KWANZA (CHANGAMOTO)
"Kama ulipo hakuna changamoto basi unaishi mbinguni." ila kama upo kwenye ulimwengu huu huu lazima mtihani huu aidha uliwahi kuufanya ukaishia njiani au kuumaliza au unaendelea kuufanya na bado huelewi idadi ya maswali unayotakiwa kuyajibu hujayajua kwasababu mitihani ya mwalimu huyu hairuhusu kwenda kujibu maswali ya mbele kisha ukaruka ya nyuma ni lazima uyamalize maswali ya nyuma ili ya mbele yawe marahisi.
Mtihani wa changamoto kila mmoja huwa ana wa kwake kutokana na kiwango chake cha kufikiri kwahiyo ukijaribu tu kuigilizia kwa jirani yako utafeli.
Mtihani huu wa changamoto unahitaji hekima wakati wa kuujibu kwani ukienda nao pupa unaweza usiumalize kuujibu. Mtihani huu huja kinadharia na kivitendo kwahiyo utaujibu kwa maandishi na utaujibu kwa vitendo ili kupata usahihi wa majibu uliyoyaandika.

2.MTIHANI WA PILI (NIDHAMU)
Baada ya kutoka katika mtihani wa changamoto unaingia kwenye mtihani wa nidhamu kwani hapa huwa kama kipimo cha majibu ya mtihani wa changamoto.Utahitaji kuujibu kwa nidhamu ya hali ya juu mtihani huu wa nidhamu kwani ndilo daraja la kukuvusha aidha kupanda au kushuka katika kitivo cha maisha.
Utahitaji kuelezea uzoefu wako wa kujiheshimu na kuheshimu wengine,kumuheshimu Mungu na Amri zake,kuheshimu muda wako na wa wengine,kuheshimu fedha unayoipata na unayoitoa kwa kukokotoa thamani na asilimia,faida na hasara,mapato na matumizi,bajeti na akiba,hazina na uwekezaji.
Nadhani ndio maana mtihani huu huwa ni mgumu zaidi kwa wanafunzi wa kitivo hiki kutokana na aina yake ya maswali na ufanyaji kwa ujumla maana hesabu kanuni na njia zake zinazidi zile za albert Einstein,Isaack Newton na wakina archmedes n.k.

3.MTIHANI WA TATU (HEKIMA)
Kama nilivyokuambia hapo awali ili majibu ya maswali ya mbele yawe marahisi hutegemeana na namna utakavyojibu maswali ya nyuma.
Mtihani wa hekima siyo mgumu kama ukifuzu mtihani wa nidhamu kwani maswali yake hufanana na hutegemeana sana.
Kwahiyo hakikisha unakuwa makini na mpole katika kutafuta majibu ya mitihani hii.
Huu ni mtihani ambao utatakiwa kuujibu kihisia zaidi na sauti zilizopo ndani yako kwani huitaji hekima,ustahimilivu na unyenyekevu.

4.MTIHANI WA NNE (SUBIRA)
Unahitaji kuwa na subira sana kuanzia katika mitihani hii kwani mwalimu ambaye ni ulimwengu huwa aidha anachelewesha au kuwaisha majibu kwahiyo hicho nacho huwa ni kipimo na swali katika mtihani huu.
Kuujibu mtihani huu unahitaji kuwa na uzoefu,mifano na kumbukumbu kwani maswali yake hulenga zaidi uhalisia na mapito na namna ulivyojifunza kupitia mapito hayo.

5.MTIHANI WA TANO (UAMINIFU)
Katika chumba cha hii mitihani daima huwa hakuna kusimamiwa na wala muda rasmi wa kumaliza kutokana na kila mtu kuwa na mtihani wake na ukitaka kufeli katika mtihani huu ni pale utakapojaribu kujibu maswali yako kwa majibu ya wengine.
Kuujibu mtihani huu inatakiwa kuwa na hofu ya Mungu kwani ndiye pekee atakayekuongoza kufanya maswali yako kuwa mepesi.
Kwa kipimo maalumu utapimwa na mwalimu ili kuingia katika mtihani huu na kipimo kikikataa wewe kufanya mtihani huu itatakiwa uanze upya kufanya mitihani iliyopita.
Maswali yaliyopo katika mtihani huu siyo yale ya "wiki hii utapokea muujiza mkubwa kama unaamini type amen" usitegemee maswali ya namna hii katika mtihani huu kwani ni mtihani nilioushuhudia watu wakiujibu kwa kulia na kusaga meno.

SASA UNASTAHILI KUVESHWA TAJI NA SHAHADA YA Ph.L KAMA UKIFANIKIWA KUJIBU MITIHANI HIYO.
Huu ndiyo wakati ambao mwanafunzi anakuwa amelegea na kuchoka kabisa na hata wengine kukata tamaa kabisa kwani sherehe ya kutunukiwa kwao huwa siyo ya mbwembwe wala miziki au sherehe ya namna yoyote ile na hakuna ambaye huwa anajua ni lini atahitimu na kutunukiwa shahada yake kwani kila mwanafunzi hufuzu kivyake na kwa wakati wake kwahiyo unatakiwa kuwa tayari kwa majibu yoyote yatakayoletwa na mwalimu huyu kwani hata ukikosea kidogo tu mwalimu hakujumuishi kabisa katika sherehe hii na atakurudisha tena mwanzo katika vyumba vya mitihani.
Pindi mwalimu anapokuletea majibu yako na kukufanyia usahihi huwa hataki kukosolewa,kubishana wala kujibizana kwani mwalimu huyu siyo mbabaishaji wala mwalimu hewa ni mwalimu aliyewafundisha mababu zako,baba zako,na kizazi chako so kuwa mpole usije ukavuruga matokeo dakika za mwisho kisha ukarejeshwa kwenye mitihani japo ni jambo lisilokwepeka ila lisiwe rahisi namna hiyo kutokea kwa kusababishwa na fikra zako mgando.

TUMAINI (FINAL HOPE)
Inawezekana huwaoni wenzako katika chumba cha mitihani hii ukaamini kwamba upo peke yako katika pitio lako na ukachana makaratasi ya majibu yako kwa hofu ya kupata majibu ya kukufedhehesha na kukukatisha tamaa.
Usifanye hivyo kwani ni mapema sana kuchukua maamuzi magumu namna hiyo tupo wengi sana katika chumba hicho kilichogubikwa na giza nene kiasi cha kutoona tunachokijibu ila imani pekee ndio tumaini letu na tunaamini tutatoka salama na kurejeshewa majibu mazuri na mwalimu wetu ulimwengu.
Endelea kufunga na kuomba,endelea kuamini majibu unayoandika ni sahihi,endelea kuamini wewe ndiwe utakuwa mwanafunzi bora pindi majibu yakirejea,endelea kuweka juhudi ya kuandika majibu yako kwa usahihi hata kama mwalimu haangalii mwandiko ye hutazama majibu tu,endelea kuitunza furaha ndogo uliyo nayo hata kama mitihani ni migumu,endelea endelea endelea mbele zaidi usipende kubaki nyuma kirahisi rahisi usikubali kuwekwa kituko na mtumwa na wale waliokwishatunukiwa shahada zao usitamani vya wenye shahada pigania shahada yako kwa hali na mali,jua na mvua,shida na raha,shibe na njaa,milima na mabonde,jangwa na misitu minene,vichaka na mapori pigana.

#MAPINDUZITIME

KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI.
Karibu sana katika darasa maalumu kwa mafunzo maalumu la KNOWLEDGE IS POWER (KIP) ambalo linakwenda kuanza rasmi tar 1/12/2018 kwa msimu huu wa pili litakaloendeshwa kwa siku 14 kwa gharama ya shilingi 7000/= tu.
Thibitisha ushiriki wako kwa hiari kwa kucomment namba yako ya simu ikifuatiwa na neno darasa au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia nambari za simu 0712 335 288 au 0719 342 214.
TUJIFUNZE PAMOJA,TUFANIKIWE PAMOJA.

pia kuna mtazamochanyafoundation group unaloruhusiwa kujiunga bure kabisa ili kupata fikra yakinifu kila siku bonyeza link hapo chini ujiunge moja kwa moja ila hakikisha una nidhamu na unajitambua.

https://chat.whatsapp.com/EM86U47uVzH9aPdGqmMuJJ

#AHSANTENI_WANAMAARIFA_NA_MBARIKIWE_SANA

Jumatatu, 19 Novemba 2018

MJUE BILIONEA WAKO LEO

MWANAMKE WA WANAWAKE ANAYEWAWAKILISHA AKINA MAMA WOTE ULIMWENGUNI KWA KUWA TAJIRI ZAIDI DUNIANI

Jina lake halisi ni Alice Louise Walton alizaliwa oktoba 7 mwaka elfu tisa mia arobaini na tisa (1949) ni binti wa SAM WALTON ambaye ni mwanzilishi wa WAL-MART  STORES INC.
Alice ni raia wa Newport Arkansas Texas marekani katika masomo yake alipita trinity university na kujipatia digrii ya sanaa katika masuala ya fedha na uchumi na baada ya  masomo yake hakwenda moja kwa moja kuitumikia kampuni ya familia yake bali alianza kupita katika baadhi ya makampuni kama mfanyakazi kutokana na elimu yake hasa katika mabenki na taasisi nyinginezo za kifedha.
Alice ameolewa na kutarakiana na waume zake mara mbili na hakuna sehemu inayomtaja alice kwamba amewahi kuwa na mtoto/watoto.
Pia alice anatajwa kama mtu mwenye mapenzi makubwa zaidi na sanaa na hata kuanzisha taasisi isiyo ya kiserikali wala faida yenye kujihusisha na masuala kadha wa kadha ya mambo ya kale kama vile taasisi yake iitwayo Amon Carter Museum ya huko nchini kwake Texas.
Nje ya maisha yake pia Alice amekuwa akiandamwa na maswahibu kadhaa ya ajali kwani zimwi hili limemuandana sio chini ya mara moja na kupelekea kufanyiwa upasuaji mara kadhaa.
Alice amekuwa akifuatia nyuma ya mwanamke mwenzake Françoise  Bettencourt almaarufu kama (mama wa vipodozi ulimwenguni) ambaye alikuwa nambari 17 akifuatiwa na Alice nambari 18 katika orodha ya Forbes na bloomberg  Alice alipanda kuwa mwanamke nambari moja bilionea zaidi duniani baada ya  aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza kufariki mwaka 2017 mpaka mwezi November mwaka huu(2018) Alice alitajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 47 za kimarekani sawa na trilioni 108 za kitanzania kama sijakosea na anamiliki hisa zenye zaidi ya thamani ya dola bilioni 11 za kimarekani katika kampuni ya familia Walmart stores Inc na hisa hizo ndizo humfanya kuwa kama mrithi mkuu katika kampuni hiyo ya familia.
Hiyo ndiyo historia fupi ya Mama yetu Alice Walton katika MJUE BILIONEA WAKO LEO iliyoletwa kwako na mtazamochanyafoundation billionaire's articles pamoja na udhamini wa Vee's Co.LTD na imeandikwa,kutafsiriwa na kuhaririwa na Mwl.Victor Ramadhan Kalinga.
Ahsanteni na mbarikiwe sana muwe na wiki jema lenye tija na faida mpaka kuisha kwake.
AMINA

Alhamisi, 15 Novemba 2018

USIOGOPE KUSHINDWA

USIOGOPE KUSHINDWA....
Ni kweli kwamba katika kuimarisha kitu chochote kile huchukua muda mrefu sana mpaka kukamilika lakini sio katika kusambaratika kwa kitu hicho huweza kuchukua sekunde,dakika mpaka masaa tu kuporomoshwa kwa ngome iliyojengwa kwa miaka zaidi ya kumi au karne nzima.

KATIKA MAPENZI
Katika ukurasa huu watu wengi tumekuwa ni watumwa wa mateso na uraibu wa athari mbalimbali kutokana na maumivu tuliyowahi kukutana nayo katika kipindi cha kupenda ama kupendwa.
Maumivu yetu yamekuwa siyo ya kukoma kwasababu tumekuwa tukiwakabidhi matabibu watutibu vidonda walivyovisababisha wao wenyewe tukiamini wanajua ni wapi walipolichipua tatizo ili waanzie huko kulitibu na mwisho tumejikuta tukipanua ukubwa na vidonda vyetu kutokana na kuendeshwa na tamaa zetu na wala siyo fikra yakinifu ndani ya vichwa vyetu.
Upo na mtu na unaendelea kuyavumilia mateso na maumivu anayokusababishia au aidha unarudia rudia kufanya kosa lile lile kutokana na kuogopa kuonekana umeshindwa.
Kushindwa siyo kushindikana na kushindikana siyo kushindwa ila moja kati ya hilo linaweza likapelekea ukawa mtumwa wa mateso milele na milele.

TUJIFUNZE KUPITIA MWANARIADHA DEREK ANTHONY REDMOND.
Derek Redmond alikuwa ni mwanariadha mashuhuri kutokea uingereza huko katika karne ya 20.Mnamo mwaka 1992 nchini hispania huko katika jiji la barcelona kwenye mashindano ya olympic huku katika upande wa riadha DereK aliliwakilisha taifa lake la uingereza kama kawaida katika mbio za mita 400. Shindano lilianza vizuri bila ya hitilafu yoyot.
Derek alipofikia mita 100.5 akiwa wa nne kati ya washiriki 10 ghafla nyama za msuli katika paja zilimshika na kumfanya ashindwe kuendelea kukimbia na akaanguka chini huku akiwa anapewa huduma ya kwanza aliinuka na kuanza kukimbia tena kwa kuchechemea na wakati akiendelea kukimbia kwa shida shida mtu mmoja alionekana kuruka wigo kutokea kwenye jukwaa la mashabiki na kuingia katika mzunguko wa kukimbilia kwenye njia  aliyokuwepo Derek na akamfuata ubavuni na kumpa msaada wa egemeo katika upande wa kushoto wa bega la Derek hakuna aliyetambua yule shabiki alikuwa ni nani na walipokaribia kufika katika hitimisho ya mbio zake shabiki yule alimuachilia derek na derek akamaliza mzunguko wake ni kitendo kilichopelekea uwanja mzima kuzizima na kisha kuja kulipuka kwa shangwe sio kwa ajili ya mshindi wa mbio zile bali ni kwa moyo wa kutoogopa kushindwa wa Derek katika tuzo za olympic derek alipata medal ya dhahabu kutokana na kitendo chake cha kutokata tamaa alichokionesha mbele ya hadhara na alipoulizwa je alimtambua shabiki yule aliyemsaidia? derek alijibu ndio yule alikuwa ni baba yangu.
Derek alishindwa kuwa mshindi lakini aliibuka kuwa shujaa wa muda wote katika historia ya riadha kwenye olympic mpaka kesho.

KATIKA MASUALA YA MAISHA NA UCHUMI
Donald trump alishindwa na hata kufilisika mara 11 katika ulimwengu wa uchumi na hata kupelekea kuporomoka katika chati ya ubilionea mara kadha wa kadha lakini hakuwahi kuogopa kushindwa bali alikuwa akikubaliana na hali halisi na mpaka kuwa mkomavu. Erick J. Shigongo wa Global Publishers wakati huu tusingemjua kabisa kutokana na kutaka kujiua kama alivyofanya bilionea wa zamani wa ujerumani aliyejirusha mbele ya garimoshi(treni) kutokana na utajiri wake kupukutika na yeye kufilisika kabisa  huyu aliitwa Mr.Adolf Merckle. Lakini Shigongo zoezi lake halikufanikiwa kutokana na watu wake wa karibu kufanya juhudi za kumuokoa kutoka katika ombwe na jinamizi hilo la kujiua hii ni baada ya kudhulumika Tshs Mil.400 alizokuwa ametaka kuwekeza katika ujenzi wa kivuko huko mkoani Mwanza ziwa victoria.
Lakini pia kumbuka yule aliyekuwa mfalme wa mchezo wa golf hapo kipindi cha nyuma maarufu kama Tiger Wood kuna kipindi aliporomoka kabisa na wengi tulifikiri huyu jamaa labda amestaafu kimyakimya au anauguza majeraha kama mkongwe Michael Schumacher wa formula 1, kutokana na dunia kumpotezea kwasababu ya kufilisika na kugubikwa na skendo na kashfa kadhaa zilizomchafua sana na hali hii ilimpelekea kufikiria kujiua lakini ikafika wakati akaacha kuogopa kushindwa na kweli akashindwa kabisa na miaka ya hivi karibuni akarejea katika hali mpya na akawa bora tena katika ulimwengu wa golf tena kwa kuzirejea nafasi zake zilezile za juu.

katika kitabu kimoja cha Robert T.Kiyosaki maarufu sana cha RICH DAD POOR DAD katika sura ya 7 kuanzia ukurasa wa 164 Robby anaelezea namna ambavyo unaweza kukubaliana na tatizo bila kuathiriwa nalo kwa kutumia falsafa ya watu wa Texas ambao hupenda kusema "when texans win,they win big. And when they lose,it's spectacular." kwa kiswahili maana yake iko hivi "mtexas anaposhinda basi hushinda kwa ukubwa.Na anaposhindwa huvutia."
Kwanini hawa jamaa jambo la kushindwa wanalichukulia ni la kuvutia? Ni kwa kwasababu huwa wanachukulia kushindwa kokote ni sehemu ya hamasa na siyo majuto katika ukurasa wa 167 unwaongelea hivi watexas "They took a great failure and turned it into inspiration" hapo ikiwa inamaanisha kwamba "Huwa wanachukulia kushindwa sana ni sehemu ya hamasa."
Huku naye Robert Kiyosaki katika ukurasa wa 166 amesema hivi "So for most people,the reason they don't win financially is because the pain of losing money is far greater than the joy of being rich." hapa tupafafanue kidogo Uncle Robby alikuwa anamaanisha nini?
alikuwa anamaanisha kwamba kwa watu wengi sababu inayowafanya wasifanikiwe kifedha ni kutokana na maumivu ya kupoteza fedha ni makubwa kuliko furaha ya kuwa tajiri."

TUJIFUNZE KWA WALIOKUWA MABILIONEA NA WAKAANGUKA.
Kila siku inawezekana ukawa unakutana na chati za mabilionea kupanda na kuwa matajiri zaidi duniani kwenye vyanzo mbalimbali vya masuala ya kiuchumi. Lakini ni vigumu kuja kuzipata taarifa za hao hao mabilionea pindi wanapokuwa wameshindwa.
Tunaposema jifunze kwa waliofanikiwa na jifunze kwa walioshindwa pia hatuna maana uende ukajifunze kwa walioshindwa kabisa kuthubutu huwa tunamaanisha ni wale walioshinda kisha wakaja wakashindwa kwani hawa huwa na hadithi zenye mafunzo nyuma yao kuliko wale ambao hawajathubutu kabisa yaani walioridhika na ufukara hawa huwa hawana ushauri wowote isipokuwa lawama na vitisho juu ya jambo unalotaka kulipigania.
Leo kwa ufupi sana nitakuletea orodha ya mabilionea takribani 12 tu ambao walifilisika kwa sababu kuu zifuatazo
1.Kuyumba kwa uchumi ulimwenguni mwaka 2008.
2.Uhaini na ubadhilifu katika masuala ya kifedha.
3.Mikopo (Madeni)
4.Makosa ya jinai
Sasa tuiangazie orodha hiyo

1.EIKE BATISTA bilionea wa kibrazili aliyekuwa anamiliki kampuni za OGX huku akitajwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 30 za kimarekani.Huyu suala la uchumi kuyumba lilimpelekea kukopa na kushindwa kurejesha na baadaye kufilisiwa.

2.BJOGOLFUR GUDMUNDSON bilionea kutokea iceland aliyekuwa kawekeza hisa kubwa katika sekta za kibenki nchini mwake mwake maarufu kama landsbanki inakadiriwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1.1 za kimarekani. Huyu kuyumba kwa uchumi kulimpelekea kuanguka na baadae historia ya ubilionea wake ilibaki katika familia yake kwa mwanae kuendelea kutetea taji hilo mpaka sasa. mwanaye huyu anaitwa THOR BJOGOLFSSON.

3.ALLEN STANFORD  wa Stanford Financial Group aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 8.5 za kimarekani huyu alifilisikia kutokana na uhaini na ubadhilifu wa fedha na anatumikia miaka 110 gerezani tangu mwaka 2009.

4.ELIZABETH HOLMES kutokea Marekani na mmiliki wa Taasisi ya afya iitwayo Theranos ambaye alijipatia utajiri wa dola bilioni 9 za kimarekani kupitia ugunduzi wa njia ya upimaji wa damu kiteknolojia akitajwa kama mwanamke mdogo zaidi kuingia katika orodha ya mabilionea ulimwenguni na kuwa katika orodha ya watu 150 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa mwaka 2015 lakini miaka miwili baadae naye alikuja kufilisiwa kutokana na makosa ya kiuchunguzi yaliyong'amuliwa na maafisa uchunguzi kupitia teknolojia yake kwahiyo faini na kufungiwa kulimpelekea kuanguka.

5.BERNARD MADOFF
Alikuwa maarufu kama mzee wa "ponzi schemes" au split strike conversion ambao ulikuwa ni mfumo wa kifedha aliokuwa ameugundua kwa ajili ya kuwaleta wawekezaji pamoja kuwekeza fedha zao kama amana yenye kupanda na kushuka ilyopolekea taasisi hiyo kuwa na dola bilioni 64.8 za kimarekani na baadae alikuja kuanguka kutokana na kuyumba kwa uchumi mwaka 2008 na mfumo huu wa "ponzi schemes"ndiyo mmoja kati ya uliompelekea ALLEN STANFORD aliyeko namba 4 anayetumikia miaka 110 jela kuingia hatiani kwa kufanya uhaini katika mfumo huu.

6.SEAN QUINN ambaye ni raia wa Ireland aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 6 za kimarekani kupitia kampuni zake za QUINN GROUP ambaye alifilisika kwa kuyumba kwa uchumi,madeni na uhaini wa fedha kupitia makampuni yake ya bima.

7.VIJAY MALLYA ni raia wa kihindi aliyekuwa akiishi nchini uingereza aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya KINGFISHER AIRLINES kampuni aliyokuwa ameirithi akiwa na umri wa miaka 28 na kuifanya  ikue kwa kutengeneza pesa nyingi zaidi kipindi ikiwa mikononi mwake na alikuwa anamiliki utajiri wa dola bilioni 1.5 za kimarekani na alifilisiwa kutokana na mikopo na madeni yaliyokuwa yakimuandama.

8.ADOLF MERCKLE huyu ni bilionea kutokea ujerumani ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa anamiliki utajiri wa dola bilioni 12.8 za kimarekani kupitia kampuni yake ya VEM na alikuja kufilisika kutokana na uchumi kuyumba mwaka 2008 na kumpelekea kushiriki katika kamari alizokuwa kawekea hela kubwa na zikaliwa na baadae mambo yalivyomzidi aliamua kujiua kwa kujirusha mbele ya treni.

9.ALBERTO VILLAR huyu ni raia wa kimarekani aliyekuwa akimiliki kampuni ya AMARANDO INVESTMENT COMPANY na anatajwa kuwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1 za kimarekani na alifilisiwa kutokana na ubadhilifu wa kifedha alioufanya  kupitia kampuni yake kwa wanahisa wake na baadaye kutiwa nguvuni yeye na mkurugenzi mwenza wake Mr.TANAKA na wanatumikia kifungo cha miaka 10 jela kutokea mwaka 2005 nadhani watakuwa walishatoka.

10.HUANG WENJI moja ya mabilionea waliokuwa adimu zaidi ulimwenguni kutokana na kujificha sana maana hata picha za huyu jamaa ni za tabu kuzipata. Alikuwa anamiliki kampuni ya CHINA JICHENG HOLDINGS na alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1.9 za kimarekani. Alifilisika kutokana na soko la hisa kuporomoka ghafla kwa 91%.

11.PATRICIA KLUGE ni mtarakiwa wa bilionea wa miaka ya 1990 bwana JOHN KLUGE aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 5 na alipata dola milioni 1 baada ya kutarakiana na mumewe ambayo aliielekeza katika biashara zake hasa za rasilimali zisizohamishika (real estates) katika kampuni ya Abramile estate/Kluge estate kwenye upande wa majumba ya kifahari aliyokuwa akiyapangisha na baadaye alifilisiwa kutokana na madeni yaliyokuwa yakimuandana.
Kampuni hii baadae ilikuja kuuzwa na kuchukuliwa na Donald Trump kwa dola milioni 6 za kimarekani.

12.RAMESH CHANDRA ni raia wa india ambaye alikuwa amewekeza zaidi katika sekta ya mali zisizohamishika na alikuwa akimiliki utajiri wa dola bilioni 9.2 za kimarekani katika kampuni yake ya UNITECH REAL ESTATE COMPANY na alikuja kufilisika kutokana na skendo ya mwanae Sanjay Chandra aliyejaribu kudukua mfumo wa mawasiliano serikalini na kutiwa nguvuni mwaka 2011 skendo hii ilimpelekea kulipa mamilioni ya fidia na faini na kumpelekea Ramesh kushindwa kurejesha baadhi ya mikopo katika taasisi za fedha zilizokuwa zikimdai.

KUMBUKA:-Tembo atakonda msimu wa njaa lakini hatorudi kuwa mdogo kama mbuzi, ninavyosema mtu alifilisiwa siyo kwamba ndiyo alirudi chini kabisa na kuwa kama mimi na wewe tunaoogopa kuthubutu au kusonga mbele pindi tunapokabiliwa na nyakati ngumu au tukikutana na majaribu pindi
tukisikiapo hadithi za kusisimua kama hizi kumbuka mabilionea ni wale ambao huanguka na kuinuka mara kadha wa kadha kama alivyoporomoka Yusuph Manji,Donald Trump kutokea nafasi za juu mpakanafasi za mkiani kwa orodha ya forbes ya oktoba mwaka huu.

KUANGUKA KUINUKA KILA MARA ICHUKULIE KAMA MALWEDHE DANCE YA KINGMONADA.
Unajua kuanguka na kuinuka mara kadhaa ni sawa na kucheza nyimbo ya kingmonada ile malwedhe dance yaani unaanguka unaumia na unainuka tena huku ukiwa huna huzuni ya maumivu ya kucheza malwedhe dance basi unakuwa na furaha kutokana na utamu wa nyimbo kwahiyo igeuza hali yoyote ya kuanguka kuinuka katika maisha kama malwedhe dance.
Tambua kuigeuza hali yoyote katika maisha ni kama malwedhe dance kwani hata ule wimbo nao utachezwa sana na kuna wakati utakwisha tu na utakwenda kuimba na kucheza wimbo mwingine katika maisha.

"USIOGOPE KUTHUBUTU KWASABABU UNAOGOPA KUSHINDWA OGOPA KUSHINDWA KABISA KUTHUBUTU"

KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI.
Karibu sana katika darasa maalumu kwa mafunzo maalumu la KNOWLEDGE IS POWER (KIP) ambalo linakwenda kuanza rasmi tar 1/12/2018 kwa msimu huu wa pili litakaloendeshwa kwa siku 14 kwa gharama ya shilingi 7000/= tu.
Thibitisha ushiriki wako kwa hiari kwa kucomment namba yako ya simu ikifuatiwa na neno darasa au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia nambari za simu 0712 335 288 au 0719 342 214.
TUJIFUNZE PAMOJA,TUFANIKIWE PAMOJA.

pia kuna mtazamochanyafoundation group unaloruhusiwa kujiunga bure kabisa ili kupata fikra yakinifu kila siku bonyeza link hapo chini ujiunge moja kwa moja ila hakikisha una nidhamu na unajitambua.

https://chat.whatsapp.com/EM86U47uVzH9aPdGqmMuJJ

#AHSANTENI_WANAMAARIFA_NA_MBARIKIWE

Ijumaa, 9 Novemba 2018

UPO TAYARI? ARE YOU READY


UPO TAYARI? (ARE YOU READY?)
KIROHO (SPIRITUALITY)
Upo tayari kunyakuliwa? au ndio kwa miaka +25 uliyofikia bado unaendekeza ujinga na anasa kumbuka hizo hela unazozifukia kwenye upuuzi huji kuzivuna zenyewe zikiwa zimezaliana maana hili ndilo zao pekee ulimwenguni ukilipanda hivi linaota vile so jiandae kuvuna majuto ambaye atakuwa mjukuu wako wa kwanza kabla hujazeeka.
And remember that around the corner JESUS is coming so jiandae unyakuliwe hasa kama uko tayari maana usafiri wa wengi haumngoji abiria ila abiria ndiye hufanya maandalizi na kisha kuungoja usafiri na  kwa ndugu zangu waislamu turejee kwenye swala kwa kumsujudia ALLAH SUBHANAHU WA TA'ALA maana BIBLIA TAKATIFU na QURAN vitabu hivi vimetuweka wazi ukweli juu ya nyakati hizi but tunajipoteza na kujifanya bize na mambo yasiyo na tija au yenye tija but tunasahau MKUU WA YOTE means we're not ready kunyakuliwa.
DO YOU WANT TO BE FAMOUS/RICH/BILLIONAIRE OR SUCCESSFULL?
JE UNATAKA KUWA MAARUFU/TAJIRI/BILIONEA AU MTU ULIYEFANIKIWA?
Je umefanya maandalizi?
Sijakosea hapo kwenye hilo swali maana unaweza ukawa na selfdoubts kwamba sasa tajiri na bilionea si ndio walewale au mtu maarufu na mtu aliyefanikiwa si sawa tu.
Hapana guys wanatofautiana kwasababu ya aidha ya kufanya au kutofanya maandalizi huwezi niambia eti MOHAMMED GULAM DEWJI au ALIKO ALHAJ DANGOTE ni watu maarufu kama unabisha muite hata dada yako au mpenzi wako au mtu yeyote yule anayeishi kama ndezi halafu muulize unamjua "DANGOTE" atakwambia acha utani nani asiyemjua DIAMOND nchi hii? hivi hujui nchi hii hii ya UNCLE MAGU zile saruji na yale malori ya rangi ya silver yenye chapa ya dangote kuna watu wanajua ni kampuni ya Diamond platnumz.
Nimewahi fanya huu utafiti majibu yake yalisababisha mbavu zangu kuvunjika fanya na wewe kama unatamani kucheka.
Kuna watu ni maarufu na hawajafanikiwa  kwa mfano dada yetu Wema Sepetu angekuwa na biashara zake kama JIDE  asingekubali kuwa kituko katika jamii kwa utomvu wa nidhamu.
Na kuna watu sio maarufu na wamefanikiwa kwa mfano Omar Msigwa mmiliki wa kampuni ya SUPER FEO na SELOUS  maana tangu nakua nayaonaga tu mabasi yake ila yeye sikuwahi kumjua na nina miaka kadhaa hapa Njombe bado sijawahi kukutana naye japo wenyeji wanasema ni mtu wa kujichanganya sana yaani yupo simple tu ila shida ni kumgundua maana unaweza ukala naye mgahawa mmoja na usimjue kwasababu siyo maarufu bali ni tajiri kwasababu alifanya maandalizi ya kuwa tajiri siyo maarufu.
ACHA KUJITIA STRESS UTAPOTEA
Ukitaka kuwa uliyefanikiwa,tajiri,bilionea na maarufu kwa wakati mmoja lazima utakuja kujuta tu siku moja.
JIFUNZE KWA MIFANO
Unamkumbuka MICHAEL JACKSON? ofcourse alikuwa ni msanii maarufu na mwenye utajiri mkubwa zaidi ulimwenguni lakini hakufanikiwa eh hakufanikiwa kwani jamaa alifanikiwa kuishi maisha ya furaha,amani na uhuru? maana watoto walikuwa wachupa,weupe wa dukani,sindano na dozi za kila siku huku behind him alikuwa under satan's administration so hapa ndiyo utaelewa wa mbili havai moja au mshika mawili moja humponyoka na likikupokonyoka shetani analidaka kisha analing'arisha na kukufanya uwe mfuasi na mtumwa wake be careful my sisters and brothers tunayewaza noti mingi mingi.
Mbali na Wacko Jacko turejee kwa Brother Stephen Kanumba ilikuwaje vile..! behind his fame? vipi nalo tuliongelee Nope tuishie hapohapo ila unatakiwa kutofautisha malengo,ndoto na tamaa.
Maana ukiwahoji vijana wengi utasikia nataka nije kuwa mtu fulani mkubwa mwenye mafanikio na ukimuuliza who is your role model? atakutajia lifuasi maarufu la shetwani instead of himself or Jesus,Mtume Muhammad,Daudi,Suleiman n.k.
Slim sal aliwahi kusema hivi nitamnukuu
"Role model wangu ni huyu nimtazamaye kila siku nikisimama mbele ya kioo"
Yah sawa jifunze kwa waliofanikiwa but not kutamani waishivyo au kujilinganisha nao wewe ni wewe na wao ni wao mbona hata wao huwa wanatuambia kila siku.
Lord eyes aliwahi kusema "nisikilize ninachokisema ila usifuate ninayoyatenda"
Fanya sana maandalizi ya kutosha katika eneo hili kwani usipokuwa makini badala ya kutoka kwenye ukata na kuelekea uhuru wa kipato utajikuta umezipata hela ulizokuwa unazihitaji halafu bado ni mtumwa vilevile.
Ngoja nikupe siri moja ukiingia youtube nenda kasearch "how money made" angalia kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho kisha toka mtandaoni halafu chukua noti yoyote utakayo kuwa nayo mfukoni au katika pochi kwa wakati huo kisha ishike kwa mikono miwili ipeleke mpaka juu kama vile tunavyokaguaga hela bandia halafu baada ya hilo zoezi anza kutafakari mimi na hili karatasi nani alianza? kumbuka kule youtube kwenye ile video kuna watu utawaona wako bize kazini so after that utagundua kwamba huhitaji majini wala shetwani kulipata hilo karatasi unachohitaji ni akili tu yaani akili iliyotumika kulitengeneza hilo karatasi na kupewa thamani basi wewe unaihitaji akili kubwa zaidi ili kuwa na hayo makaratasi mengi ili kiwanda kiwe bize zaidi kwa ajili yako kwasababu hebu just imagine wewe mwenzangu hivi ni wapi uliwaona machizi wanatafuta hela? Ndio maana daily tunasema utajiri wa kwanza ni akili but not otherwise.
ACHA KUFANYA MAANDALIZI YA KITOTO
(STOP DOING THE CHILDISH PREPARATION)
Kama una kaubongo kaliko jaa umbea,picha za ngono,list ya girls/boys,alcohol, na upuuzi wowote ule sure i'm telling you utafanya tu vimaandalizi vya kitotototo, vimaandalizi hivi ndio vile vya kuwaza hili mara lile kila siku unajipa excuses na kuhairishahairisha mambo
Tumaandalizi twa kitoto ndio tule ambato tunatutesa vijana wengi kutafuta njia rahisi ya kutatua matatizo magumu.
Maana nowadays sio siri kila kitu unachokifanya au utakuja kukifanya wewe ili upate pesa nyingi sema tu "kwa urahisi" au "kwa muda mfupi" kwa mfano kwa ndugu zangu mnaoendesha blogs na platforms mbalimbali kujiingizia kipato mnatumia sana hizi kauli nitawanukuu
"Jinsi ya kupata hela kwa urahisi"
"Jinsi ya kupata chochote unachokitaka ndani ya muda mfupi"
"Jinsi ya kufika kileleni haraka"
"Jinsi ya kupata six packs kwa siku 28 tu"
"Jinsi ya ku............. kwa njia rahisi"
kwa misemo hiyo kwanini wanaojiita manabii wasipige hela kwanini waganga wasitajirike kwanini bloggerz na youtube channel owners wasipate views na pesa nyingi kiurahisi? sasa vimaandalizi vyako vya kitoto ndivyo vitakufanya uwatajirishe wengine na wewe ubaki fukara maisha yako yote.
FANYA MAAMUZI NA MAANDALIZI IMARA
(MAKE STRONG DECISIONS & PREPARATIONS)
Ukiwa na maandalizi ya kutaka kuja kufanya vitu vikubwa ni lazima uambatanishe na maamuzi imara.
Kelele za ndugu na jamaa fyekaaa
kelele za mwenzi au mpenzi wako fyekaa
kelele za majirani fyekaaa
kelele za wanaosema utashindwa fyekaa
kelele za wanaokufanyia ubaya kwa makusudi ili ukate tamaa fyekeleaaa mbali.
Kelele za tafiti za kipuuzi zinazoitabiri kesho yako mbovu nazo fyekelea mbaliii
Hizi kelele usipokuwa makini sometimes haziji kama kelele but hujaga kama ushauri, au vijimaneno vya kukutia moyo kupitia wale watu ambao unawaamini sana kumbe ni mashwetani yaliyo valia mabawa ili kuyatambua haya acha kutumia milango yako mitano ya fahamu uliyofundishwa shuleni unapaswa kutumia mlango wako wa sita wa fahamu ambao hutumika sana na vizazi vya ulimwengu wa roho nakusisitiza tena "you have to be very very careful"
Inawezekana hunielewi au unanielewa nusu nusu kutokana na taarifa hizo za kuukanganya ubongo wako right?
Usipate shida sio lazima tuelewane leo we endelea tu kunifuatilia kuna siku aidha ulinielewa,umenielewa au utakuja kunielewa.
KITU UNACHOTAKIWA KUJUA NI KWA KIASI GANI UPO TAYARI? NAIPENDA SANA KAULI YA VODACOM WASEMAYO.
"YAJAYO YANAFURAHISHA JE UPO TAYARI" hii ni kauli kubwa sana ukiifikiria kiupana ila ukiifikiria kitotototo tu "YAJAYO YATAKUFURAHISHA" tena "UTAFURAHI KWELI KWELI"
#ACHA_KUWA_NYUMANYUMA_KUWA_TAYARI_UUONESHE_ULIMWENGU_MAAJABU
Naitwa Mwl.Victor R. Kalinga wa Mtazamochanyafoundation nipo mkoani  Njombe napenda kukuona ukifanikiwa katika kila sekta siyo kifedha tu bali kuanzia ndani yako mpaka mazingira ya nje yanayokuzunguka ndiyo maana huwa napenda kukuandikia makala hizi kwa hisia kali na mifano ya kweli sitaki nikurubuni kwasababu ulimwengu una mengi nayo mengi hayana maana so yote unatakiwa kuyajua ili uyachukue yaliyo na tija na kuachana nayo yasiyo na tija ili uishi maisha ya amani,upendo,uhuru na furaha tena ya kumtukuza Mungu wako kwani ukijiingiza kwenye mkondo mbovu hata kizazi na jamii inayokuzunguka nayo utaigharimu.
Usiache kuomba,kufunga na kumtumikia Mwenyezi Mungu kila wakati kwasababu huwa hamtupi mja wake hata siku moja.
KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI.
Karibu sana katika darasa maalumu kwa mafunzo maalumu la KNOWLEDGE IS POWER (KIP) ambalo linakwenda kuanza rasmi tar 1/11/2018 kwa msimu wa kwanza litakaloendeshwa kwa siku 14 tu kwa gharama ya shilingi 7000/= tu.
Thibitisha ushiriki wako kwa hiari kwa kucomment namba yako ya simu ikifuatiwa na neno darasa au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia nambari za simu 0712 335 288 au 0719 342 214.
KARIBU TUJIFUNZE PAMOJA NA UNGA MKONO UZALENDO.
pia kuna mtazamochanyafoundation group unaloruhusiwa kujiunga bure kabisa ili kupata fikra yakinifu kila siku bonyeza link hapo chini ujiunge moja kwa moja ila hakikisha una nidhamu na unajitambua.
https://chat.whatsapp.com/EM86U47uVzH9aPdGqmMuJJ
#AHSANTENI_TANZANIA