Jumapili, 23 Juni 2019

Shule nyingi zipo mjini,ila kuwa makini sana ukiambiwa mjini shule.

Mjini kuna mengi ninayojifunza kila siku tangu nitoke mufindi nyororo kisada ndanindani kule na nikajua kumbe mjini kuna:-
Kutafuta riziki
Kutafuta maisha
Kubangaiza.


Wengi tulioingia mjini kwa lengo kuu la kutafuta maisha tumebaki kuwa wabangaizaji na watafuta riziki mpaka tunapoteza maisha sasa tujitathmini upya na mapema sisi ambao tunaelekea kupoteza maisha na bado tumekomalia ubangaizaji.
Maana kama hatukukosea kuisoma vema kanuni basi tulijibu bila kusoma swali la mwalimu Kashindi Edson lile lisemalo ulikuja kufanya nini hapa duniani?

Mjini kuna wenye mipango ya kutafuta hela,kuna wanaotafuta hela ya malengo na kuna wanaotafuta hela kwa ajili ya pango,jiangalie sana usije ukajichanganya na kutumbukia katika tundu la simba angali wewe ni nyumbu.
Mjini kuna njia za waenda kwa miguu na barabara kuu sasa ikiwa utaendelea kufurahia taa za kwenye njia za waenda kwa miguu ukiamini kwamba serikali inawathamini raia wake kumbuka kamwe hutokuja kutumia kodi yako iliyotumika kujenga na kuimarisha lami ili wewe uje utembelee chombo cha moto.
Mjini kila mmoja kivyake ndio maana muda wa kula ukifika kila mmoja humuoni alipoingilia maana ni tofauti kabisa na atakapokuja kutokea, sawa na safari ya mafanikio tu huyu atawahi na huyu atachelewa hiyo yote ni kutokana na mtu alipoingilia.
Mjini kuna wenye suti na ni smart na kuna wenye akili smart na hawana suti ila nao smart vilevile.

Mjini kuna wadada na wasichana,kuna masister na watawa pia wapo akina mama na wanawake hawa wote ukitumia nguvu kuishi nao utapoteza kila kitu pamoja na nguvu zenyewe.
Mijini kuna biashara na kuna bihasara uchaguzi ni wako aidha ufungue ofisi utengeneze hela au ufungue kijiwe ukashinde kila siku.

Mjini ni mwiko kumuuliza mtu kapata wapi pesa lakini inaruhusiwa kujifunza na kuuliza namna ya kupata pesa.
Mjini bilioni zipo mifukoni mwa watu ila kama za mfukoni mwako zikikushinda kutunza ili zivute za nje basi jua bilioni za nje ndio zinavuta elfu zako.

Mjini sihami maana kila kitu ni rahisi sana kwani ukichoka kulala peke yako unaruhusiwa kulala njaa na usipofanya kazi unakula jeuri yako huku ukishiba faida jua kabisa umekula hasara.
Mjini msiba fursa,kuoa fursa,harusi fursa,kesi fursa,maradhi fursa,ujinga fursa,umalaya fursa,uhuni fursa,taka fursa,sifa fursa,kiki fursa, yaani kila kitu ni fursa ila akili ni ghali zaidi ya ujinga ndio maana mtaji umekuwa changamoto kuu kwa vijana kuchukua fursa.

Mjini kuna Mengi yaani Mo kwa kiingereza ila bado ni mtiti kumpiku Bakharesa.
Mjini kila mtu ni tajiri na ana kila kitu ila tu vyote anavimiliki ndotoni ndio maana akianza kuota anaishia kuvipiga picha na kupost instagram kisha yeye kubaki fukara kwa kukosa usafiri na vibali vya kuhamishia katika maisha halisi.

Mjini kosa kubwa ni kumuamini mtu kwani watu wamezidi kuwa wachache zama hizi na viatu ni vingi kwahiyo chunga sana usije ukavaa cha kukuvaa kisha ukaupoteza utu.
Mjini kila mmoja ni CIA ndio maana kila taarifa wanazo kwahiyo ukija hakikisha hasira zako umeziacha nyingi ulipotoka na huku umekuja nazo hasira chache za kutafutia maisha tu ili usije ukapanic wakati wa kurelax.

Mjini kichwa usibebe kama pambo 
KAMA ningali
Kama ningali rejea utotoni basi nisingelifanya utoto ningali mtoto.

Mambo mengi ambayo huwa yanakuwa yanaanza kuonekana yanakwenda kombo huwa tunayaficha nyuma ya kauli "KAMA ningali" ili kuonesha na kudhihirisha dhahiri kwamba ni kweli tumesukumwa na hali fulani kushindwa kulitimiza jambo fulani.

KISA CHA KIJANA
Kijana mmoja mtanashati anayeishi katika nyumba ya wazazi wake iliyo nzuri ndani na nje ikiwa ina bustani ya kupumzikia na ina eneo kubwa linalowezekana kufugia mifugo midogomidogo.
Kijana huyu ana elimu ya chuo kikuu na alitunukiwa shahada ya utawala wa biashara huko chuoni CBE Dar es Salaam barabara ya bibi titi mohamed kijana alizawadiwa zawadi kemkem wakati akihitimu na moja ya zawadi hizo ilikuwa ni simu ya rununu tanashati aina ya Samsung Galaxy S9 ya mwezi machi mwaka 2018 toleo la kwanza inayogharimu kiasi cha shilingi milioni 2,300,000/= za kitanzania.
Kijana anamiliki wapenzi wanne watatu ndani ya mkoa na mmoja yupo nje ya mkoa na wote anawasiliana nao kwa pesa ya vocha kutoka kwa baba yake anazompatia kama nauli na vocha pindi aendapo kutafuta kazi baba yake ni mtumishi wa halmashauri.

Lakini kjana anatamani sana kuianzisha biashara yake kwani ana elimu nzuri ya biashara lakini kijana kila siku husema "KAMA NINGALIKUWA NA MTAJI BASI NINGALIANZISHA BIASHARA YANGU."
JE KIJANA ANAHITAJI MTAJI WA NINI ILI AANZE KUFANYA BIASHARA?

Kama ningali na-jua ningeliishi sayari ya peke yangu.
ULIMI
Ni heri ya ule ulimi wa mtoto anaoupeleka juu ili kulamba chumvi ya kamasi,kuliko ulimi wa kijana unaoshuka chini kulamba chumvi ya mgodini.
USINIULIZE TUNAKWAMA WAPI?


Ulimi mchafu hauwezi yanena mema ya maendeleo hata siku moja,ulimi mchafu hunena mabaya na kueneza chuki, ulimi mchafu huongeza chumvi katika kila neno kutokana na kuwa na chumvi chumvi nyingi za uchafu za mwili na akili.
Ulimi huleta ufukara ukiendekezwa kuwa huru kutoka kila utakapo na hasa katika kuropoka,kubwabwaja,kubishana,kutusi,kukaripa,kusengenya,kufoka,kulaghai,kudharau na kukejeli.
Ulimi huleta ufukara ikiwa kila umuonapo binti unataka kusema jambo la ushawishi ili kungonoka tambua daima uwekezaji wa chini chumvini hauwezi kukuweka juu labda juu ya kitanda ili kukufikisha kileleni.
Lakini kwa matumizi sahihi ya ulimi ndio yatakupelekea kuanza uwekezaji wa kuanzia chini katika uthubutu wako na ndio utakaokupelekea kuwa juu katika kilele halisi cha mafanikio.
Ulimi haukatai kulambishwa Rizla na jana tulikubaliana itakuwa mwisho wa kuvuta bangi,Ulimi kila pafu unapokea na nikianza kuleta fujo ulimi unajificha, ulimi hutaki niache sigara na pombe kisa unanilaghai ndio starehe zangu huku majuto yangu uzeeni.

Ulimi hauna mfupa na unavunja ndoa.
Ulimi hauna miguu na unaeneza chuki.
Ulimi hauna mamlaka na unawadharirisha wenye mamlaka kuongea pumba.
Ulimi haushiki bunduki na unaua.
Ulimi haujui kujiunga lakini bado unaleta tafrani mitandaoni.
Ulimi hulimi na bado unakula vya mjini
Ulimi hauna vyeti wala shahada na bado unawalaghai wasomi.
Ulimi hausimami lakini unatusimamisha wanaume
Ulimi unakopa na marejesho unakususia.
Ulimi unakiponza kichwa na kujificha tayani.


Ulimi wa fukara ukinena ya busara ulimi wa mwenye hadhi hupinga na kuziita roporopo.
Ulimi wa muhuni hata ukiwa unanena mema unaonekana hauna hoja kwasababu kila baada ya neno ni tusi na kila baada ya tusi ni neno.
Ulimi wa dalali na mfanyabiashara ndio ofisi yake na utupu wa kichwa chako ndio faida yao.
Ulimi wa malaya ni sumu ya akiba na malengo yako.
Ulimi wa baharia ni hatari kwa kijana mpenda vya bure..


HATUJAPOTEZA MUDA
Ni lazima tujue kuvikanya na kuvimudu vitu vidogo vidogo ili vikubwa vije vidumu visije vikaponzwa na tabia hatarishi zinazosababishwa na ulimi.
Jua kujizuia,Jua kujifanya mjinga,Ficha werevu mbele ya wajinga ila usiache kujifunza na kuwapa maarifa,Usiache kujifunza ili ufundishe,Usiache kuonya na kukemea yale maovu,usiache kujitenga na hatari ili kuepusha madhara makuu katika maisha yako.
Nena mema na kemea panapobidi,Sisitiza hofu ya Mungu,wakumbushe amri,waambie bado tu safarini na wasijisahau maana dunia ina mwenyewe.

NGOME
hakuna anayekomaa na kutarajia kuwa gome bali katika kuwa ngome ugome hutokea.

Inabidi ukae mbali na maji na moto kipindi unajikaza kisabuni kwani maji yatakuacha povu na moto utakuyeyusha.
Maisha yanaweza kukufanya kuwa gome katika safari ya kupigania kuwa ngome.

Kuwa ngome ili kuacha alama ni lazima ukumbane na watu wengi wanaotaka ubaki kuwa gome, yaani wakikuhitaji kama kuni wanakubandua na kukukoka kisha ubaki majivu na wakutupe na wakikuhitaji kama chambo watakukatakata na kukuacha vipande vipande uwakiwe na jua ukauke na ukatike zaidi.
Ngome inajengwa taratibu kwa weredi na kwa ustadi maana ngome ikisimama daima huwa hairudi chini.
Watu wengi wamekuwa magome kwasababu ya kukata tamaa mapema kwasababu ya ngome zao walizokuwa wanazijenga kuyumbishwa na maoni au ufundi mbovu wa mikono yao au mikono ya mafundi waliojinadi ni mahodari na mwisho wa siku wakaleta nyufa katika ngome yako.
Ngome ikisimama husimama daima na huwa haiyumbishwi na upepo au dhoruba jifunze katika ngome ya Yesu kule mombasa.


NGOME NI
Ngome daima ni ngome yaani
Ngome ni msimamo ndani ya nafsi yako
Ngome ni imani na ngao katika maisha yako.
Ngome ni udadisi,kuongeza ujuzi na maarifa.
Ngome ni uthubutu na kuutenga uoga.
Ngome ni kusimamia unachokiona miaka kadhaa mbele hata kama hali ya sasa haikuoneshi matumaini yoyote.
Ngome ni kinara na mfano wa kuigwa kwa jamii yako.
Ngome ni kuishi ndani ya mfumo salama,amri za Mungu,hofu ya Mungu,Maandiko na kuwa kioo cha jamii kwa jamii yako.
Ngome ni kuwa nuru kwa waliopo gizani.
Ngome ni kuwa mfano wa kuigwa na mshiriki wa ujenzi wa maadili mema kwa kizazi chako.
Ngome ni kutetea, kukemea, na kusihi panapobidi.
Ngome ni yule twende na sio tanguliane mimi nakuja. 
Ngome ni yule aliyejengwa kwa mwamba chini daima yupo imara hata kama juu watamuona dhaifu.
Ngome ni mjanja kwasababu anajua nini afanye na kuijenga heshima.
Ngome ni msafi wa mwili na msafi zaidi wa akili kuliko wa mavazi ngome sio kuvaa kwa ajili ya kuwatega wakina joel au wasafi wakina joel wapendeze wawanase wakina lili kisha waambukizane upungufu wa akili.
Ngome ni Jambia la maarifa likizungushwa linaizungusha dunia na likiachiwa linaachia maarifa kwa dunia.


NGOME SIO
Ngome sio mchizi boti wa kuniomba hela kipindi nikiwa fukara kisha nikimnyima adai nina roho ya kutu na hila.
Ngome sio mchizi boti anayenipa hela kila wakati ninapomuomba hela, ngome ananipa njia ya kupata hela ili niwe nayo siku nikiwa sina hela.
Ngome sio yule aliyekujua ukiwa na meno thelathini na mawili halafu anakuita damu yako na ukitoka anauza siri zako, ngome ni Baba na mama au walezi wako wanaoyajua madhaifu yako na bado wapo juu yako kukutetea.
Ngome sio yule mpenzi wako aliyekugeuza mgodi kisha moyo akauacha na mashimo ngome ni yule aliyekuja kufukia mashimo na bado hajali hali yako yeye kasimama imara daima kwa ajili yako.
Ngome sio mropokaji lakini ni msemaji mwenye hekima na akisema anasema kilicho wima.
Ngome sio yule anayeandika upuuzi kila anavyojisikia ngome ni yule akiandika anaandikia kwa mataifa na maarifa yanawainua.
Ngome sio yule anayeamini katimia kwa kila eneo na kujitapa,ngome ni yule anayejua kila siku anaamka mjinga na analala mwerevu kwa kila alichojifunza siku nzima.
Ngome sio yule anayeigawa jamii kwasababu ya udini,ubepari,ubinafsi,wivu,jina,rangi,wadhifa,imani,maarifa,elimu nk ngome daima anaupigania usawa.
Ngome sio teja,mlevi,mzinzi,mlafi,mchoyo,mwizi,mjinga na muuaji ngome ni kuijua kweli,kuiishi na kuieneza kwa kila mmoja ili dunia iwe sehemu salama.
Ngome sio yule aliye na sifa zote nilizoziorodhesha hapo juu lakini kila siku anajitahidi kuufikia usafi na kujipendekeza kwa Mwenyezi Mungu.

Mimi ni ngome,wewe ni ngome sisi sote tukiungana tunaweza kuijenga ngome imara lakini kwakuwa tumeambatana na magome na mang'ombe ndio maana tunabaki kuendelea kuonekana mafala.


Ungana nasi bure kabisa ili kujipatia maarifa ya kila siku kwa kuzingatia nidhamu na hekima tu kupitia group letu la whatsApp kwa kugusa link hapo chini.
KARIBU SANA
MANTA HOFU
Bora ukaogopwa kwa ujasiri wako kuliko uchekwe kwa ujasiri kwasababu ya woga wako.

Msanii Bobby McFerrin katika nyimbo yake ya don't worry be happy katika moja ya shairi lake alisema 
"In every life we have some trouble but when you worry you make it double"
Akiwa anamaanisha 
"Katika kila maisha tuna matatizo fulani na unapoyaogopa ndipo unayazidisha mara mbili."
Kisha akaimba kwa unyenyekevu na utulivu wa kiutu uzima kiitikio chake kisemacho "Don't worry, Be happy." yaani "Usiwe na wasiwasi,kuwa na furaha." 
Kwa kilahaja za kiswahili ni kiarabu,Kingazija na kiunguja twasema MANTA HOFU!

Umri unakimbia hujachumbia,hujaoa/hujaolewa huna mtoto,huna kazi,huna mtaji,huna biashara wala huna elimu.
Rafiki MANTA HOFU kuna Mungu juu aliyetuahidi huwa hawahi wala hachelewi.
Kumbuka Ibrahimu na mkewe Sara walipewa mtoto wakiwa na umri gani?
Ulishawahi kumsikia Kroc,Ford,Sanders wao walipewa ubilionea wakiwa na umri gani vile?

Hivi unakumbuka Mo dewji alivyoshindaga kwa kishindo kula za maoni jimbo la Singida mjini mwaka 2000 halafu akaambiwa we bado mdogo kaa kando kwanza kisha jimbo likaenda kwa mwingine lakini 2005 haikuwa mbali alikuja akachukua kijiti chake maana ilipangwa iwe na kweli ikawa, kwahiyo hata kwako pia unatakiwa kuMANTA HOFU rafiki zamu yako ipo tu.
Samahani rafiki hivi si umeusikia wimbo wa Harmonize Never Give up anasema alikuwa anapenda sana mpira lakini alijaribu na muziki na alivyotua tu BSS wakamwambia hana kipaji hivi angekata tamaa na kurudi tu kusakata kabumbu kwenye ndondo leo tungemjua kweli? Hata wewe Ally Rhymes ndiye unayefuatia mkuu kwahiyo MANTA HOFU juu ya fungu lako zamu yako ipo umaarufu wako upo.
Kumbuka Shigongo aliwahi kupoteza mil.400 bei ya Zhongtong moja new model mpya kabisa mpaka na chenji ya Toyota Allex mbili inarud kwa ajili tu ya kutengeneza kivuko cha kutumika Ziwa Victoria lakini mpaka leo hakijakamilika mkandarasi alimdhulumu Bw.Erick alitamani hadi kujiua lakini baadae AliMANTA HOFU na maisha yakaendelea.
Ukiingia kwenye tovuti ya Forbes utakutana na orodha ya mabilionea 10 waliofirisika kabisa kipindi kile uchumi ulipoyumba wengi walipanic,maana kuna wanaotumikia vifungo virefu jela na wengine walijiua lakini Trump alitakiwa awe miongoni mwao ila aliMANTA HOFU leo huyu hapa!.
Hivi kipindi kile mabasi hayalipi unajua Sumry alipaki yote 80,Ilasi naye alipaki na Ottawa wa songea nae alipaki yote kwa ajili ya kuMANTA HOFU tu hawataki presha hawa jamaa hata kidogo ila leo Ilasi huyu hapa karudi,Sumry yule kule shambani na Ottawa anakomaa na vituo vyake vya mafuta naye kuna fununu atarudi siku sio nyingi.
Sasa wewe una mpenzi tu yaani hata ofisi huna lakini unaumizwa,unanyanyaswa, unachunwa, unasemwa mpaka unakonda mkuu halafu hutaki kuMANTA HOFU kisha ufanye mambo mengine.Onhoo! kama hutaMANTA muda huu ukiwa kijana basi jua mbeleni shida ndio zitakuMANTA.

Hivi unajua Emmanuel Elibariki almaarufu kama NEY WA MITEGO aliunguliwa na chumba alimokuwa anaishi kile kipindi cha Hellouw My love na kupoteza kila kitu pamoja na kuziliwa kale katoto kake kasuriama, unajua alifanyaje? aliMANTA HOFU akakaa sana Iringa pale baadae akarudi upya ndio huyo mpaka leo.
Jifunze kwamba kuna wakati utapoteza kila kitu ili kupata vitu zaidi.

Nakusisitiza sana mkuu/mheshimiwa/mwanamaarifa na rafiki yangu wa kweli kwamba hata iweje hata yaweje MANTA HOFU kama ni kipindi kigumu basi kitapita kama ni matatizo basi yatakwisha na kama ni changamoto jua ndio zinakukomaza na kukuandaa shujaa jasiri na mwenye nguvu pindi ukija kulitwaa kombe lako.
Jiamini
Jikubali
Jifunze
Jitunze
Jipende
Jipe moyo
Jitume
Jithamini
Jitahidi
Jimudu
Jipendelee.


UNGANA NASI
Karibu katika mtazamochanyafoundationgroup tujifunze zaidi bila ya gharama yoyote kwa kubonyeza link hii tiketi yako ni nidhamu,kujitambua na kupenda mabadiliko

AHSANTE SANA


NJIA
PENYE NIA PANA NJIA,PANA NJIA SIYO NDIYO NIA.
Kati ya kazi ngumu inayotushinda na kutupelekea vijana wengi wenye ndoto na malengo makubwa kuishia njiani ni katika maandalizi ya uundaji wa njia bora kwa ajili ya watu watakaotufuata nyuma yetu.
Yabebe malengo yako kama sululu, ibebe ndoto yako kama beleshi na yaambatanishe maono yako kama jembe, Vaa mabuti ya ujasiri na jiveshe glavu za uthubutu kisha kachimbe na kuiunda vema njia yako.

VIJAMBO VIUNDAVYO NJIA KUU NA NJEMA
Nina vijambo kadha kwa siku ya leo katika kusaidiana kwenye ujenzi wa njia na upanuzi wa kile tunachokipigania katika maisha yetu.
 
JAMBO LA KWANZA
Ili iwezekane kwetu kuiunda njia ni lazima tuibebe imani ndani yetu hata kama itakuwa ni kubwa kuliko umri wetu na nzito kuliko uzito wetu lazima tukubali tu kuibeba.
Imani zetu hupotea pale pahala unapofikia wakati wa kila mmoja wetu akionekana ana mtoto na siye hatuna,kila mmoja wetu ana mke na siye hatujui hata mahari yalipwaje,kila mmoja wetu anaonesha kuanza kufanikiwa nasi twazidi kuparamiwa na hasara na kufirisika hata kabla ya kutajirika, ule wakati siye ni mahoehae na twaonekana mazube kwa kuamini mitazamo chanya yetu huku wengine wakifanikiwa haraka haraka kupitia waganga,kamari,kubashiri na kuuza hata visivyo halali.
Hizo ndizo nyakati ambazo vijana wengi huziacha njia zetu na kwenda kuzijaribu njia za mkato ili tu tusionekane tumeshindwa huku tungekuwa na imani kuu ndani yetu tungeamini kwamba kushindwa ni sehemu ya kujifunza tu na tungeendelea na kuunda njia zetu.
JAMBO LA PILI
Tunapokwama ni pale magumu yanapokuwa yamesongamana njiani kiasi cha kushindwa kuona mbele.
Ni ngumu kumwambia mtu aliyekata tamaa asikate tamaa huku tayari tamaa alikwisha anza nayo awali kabla hajaanza kuikata.
Vijana wengi tupo hivyo huwa tunaanza kwa kuwa na tamaa kubwa katika uundaji wa njia kisha ikianza kukatika nasi twakatika katika na kusawajika kabisa kiasi cha kushindwa kuokoteka maana tayari msongo na mfadhaiko vinakuwa vimeshauvaa uhuru na amani yetu.
Nataka ninene na ngoma zako za pina kisha nipenye katika pinea yako ili usisahau kirahisi kwamba:-
Karibisha kila kitu katika maisha yako ila hakikisha unakaribisha vya msingi pekee katika fikra zako ili uwe imara katika kupambana na hofu maana kuna pahala utapachimba na kuinuka na nyoka na pahala bee utapachimba litainuka jiwe na kukuumiza hiyo haitamaanisha utupe zana na uache kuiunda njia
JAMBO LA TATU
Epusha kabisa ubwabwajaji ovyo katika uundaji wa njia yako.
Hakuna wawili katika kuunda njia moja tambua njia yako ni yako tu na yake ni yake tu.
Kinachotukwamisha wengi ni kuwashwa kusemasema mambo yetu kwa kila mmoja hata kwa wale walioshindwa kuziunda njia zao unategemea utapata nini kama sio kubezwa,kukejeliwa, kukatishwa tamaa na hata kupingwa.
Jifunze sana kuiunda njia yako katika ukimya kiasi cha kuepusha hata zana zako zisigongane pindi uchimbapo kuiunda vema njia yako.
Ibebe sana imani ya Mwenyezi Mungu ndani yako katika kuiunda njia yako maana ulimwengu wa sasa una mengi hasa ukionesha una mengi ya kuyafanya.
Kumbuka katika kitabu Yohana 14 mstari na aya ya 6 maandiko yanasema
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
No photo description available.

Jumatano, 19 Desemba 2018

FOURTHFALSEWORLD

FOURTHFALSEWORLD
DUNIA YA NNE YA UONGO
Kila mmiliki wa mtandao wa kijamii akihojiwa nini nia na dhumuni la kuanzisha mtandao wa kijamii? huwa anasema ni kwa ajili ya kuwaleta watu pamoja.
Swali ni je umeletwa pamoja au umeletewa hoja ya uongo ya pamoja?

Lakini swali hilohilo tukiulizana watumiaji je tumeletwa pamoja kweli? nadhani majibu yatatofautiana right?

Labda mimi nianze kwa upande wangu kutokana na experience yangu ya kutumia mitandao ya kijamii kwa muda mrefu sasa.

Ukiniuliza mimi sasa nitakujibu kama ifuatavyo tena kwa ufupi tu maana kwa urefu hatutomaliza leo.

MAJIBU:-
Nauona umoja wa uongo katika dunia hii ya nne ya uongo,naona maisha yetu ya uongo ndani ya dunia hii ya uongo,naona kundi langu la uongo la marafiki 4000 na ushee waliombatana na mimi kiuongo pia najiona mimi ni miongoni mwa rafiki wa uongo kwa baadhi ya marafiki zangu ambao wanaendekeza uongo katika ulimwengu huu uliojitenga na uhalisia,Naona picha nasioni maelezo ya kweli juu ya uhalisia kwahiyo nao ni uongo pia,naziona video za utupu na kufuru mtandaoni kitu ambacho sikioni mitaani kila nikijaribu kupeleleza ili nikiweke sawa,nawaona marafiki zangu wakiwa kwenye mahotel makubwa,majumba ya kifahari na magari ya kisasa na wengine kwenye ndege kabisa lakini nikikutana nao nakumbuka kuwa sharti la dunia ya nne ni lazima usiishi kama unavyoishi dunia ya tatu so? ni uongo pia au?,
Nawaona marafiki wanaotuma picha wanakula vyakula vya ghali na nikigeukia majumbani mwao nasikia kelele za wadogo zao wakigombaniana nani ale kichwa nani ale mkia,Nayaona mapenzi ya dhati mtandaoni wapenzi wanapokutana katika dunia hii na siioni furaha yao katika uhalisia,Nayaona mapenzi ya uongo pia yanayoanzishwa na kufia hukuhuku katika ulimwengu wa uongo bila ya watu kukutana na mmojawapo tayari keshatapeliwa,Nawaona marafiki wanaotuma picha wakiwa wamevalia nguo mpya kila siku mtandaoni na tukikutana uraiani nakumbuka walikuwa wakifanya biashara za marafiki zao wenye camera na maduka ya nguo,naonana na ndugu na jamaa kila siku nikiingia katika ulimwengu huu na tukikutana husema aidha wamenisahau au hata wanaonikumbuka huniuliza mbona huonekani siku hizi? umekuwa adimu best..!! nikakumbuka kumbe ninaedit sana picha kuonekana nimeng'aa kumbe nimepaushwa na dhiki na baridi la njombe,naona picha za watu waliofariki wakapostiwa na ndugu zao wa karibu bila ya kuombwa ridhaa zao pindi walivyokuwa hai na watoa maoni hutoa maoni yao kwa kutetema na kuhuzunika kwa kuandika RIP na wengine jinsi walivyo waongo zaidi hulike vifo hivyo huku wao binafsi wanaogopa kufa sasa najiuliza wanalike nini?,Naliona kundi la watu lililojitenga na uhalisia na kuishi ndani ya mfumo wa dunia ya uongo na hata kubadili majina yao kujiita majina ya kike na wanawake kujiita ya kiume kwasababu wanazozijua wao wenyewe binafsi,Nawaona waandishi wenzangu tunaojitahidi kuielimisha na kuihamasisha jamii kila siku na bado dunia hii na watu wake inatupiga vita tusivifikie vizazi vyao zaidi,Nawaona ndugu jamaa na marafiki ambao wanaongea zaidi kiingereza mtandaoni huku uraiani ukiwasalimia tu hawataki kukujibu kwa lugha ya kiingereza wanayoiongea katika ulimwenguni huu,bado nawaona wakituma picha wakiwa wameonesha sehemu za nyuma za miili yao huku wakiwa wamevaliwa mavazi ya ajabu kwa ajili ya comments,followers,likes,viewers,shares n.k huku nikigeuka ulimwengu wa tatu muda wote wana vitenge maungoni,Naziona ajali nyingi katika ulimwengu wa tatu zinazosababishwa na madereva ambao huendesha vyombo vya moto huku wakiwa ulimwengu wa nne,Nawaona wanaharakati wanaokemea maovu kwa kupaza sauti wakiwa ulimwengu wa nne na wakirudi ulimwengu wa tatu huambatana na maovu wanayoyakemea,Nayaona madarasa mengi na sioni walimu katika ulimwengu huu,nawaona madaktari na sizioni tiba,nawaona mafundi na sipati huduma stahiki,naziona bidhaa na biashara nyingi za kupendeza katika ulimwengu huu lakini nikizinunua hazifanani na wakati mwingine sizipati kabisa,naziona ripoti na takwimu za uongo ambazo kila siku zinasambazwa na kuvifanya vizazi vya kutafuniwa viamini katika uzushi,Naziona  chuki na wivu vikishamili ndani ya ulimwengu huu wa nne kutokana na uongo uliopo ndani yake,tambua naona pia kuna ubaguzi na unafiki katika mengi yatendekayo katika ulimwengu huu wa nne wa uongo.

ULIMWENGU WA NNE WA UONGO NI KAMA BLANKET NZITO KWA WAAFRIKA NA WAJINGA WOTE ULIMWENGUNI.
Wanasema aliyelala usimuamshe kwani akiamka utalala wewe je unaujua upande wa pili wa msemo huo? uko hivi:-
aliyelala usimuamshe bali muongezee joto.
Jamii zetu za kiafrika zinasubiri birthdays kwa hamu na shauku kubwa kuliko tunavyomsubiri Masihi na ukombozi kabla ya siku ya kiama.
Walianza taratibu kutujaribu kwa masuala ya sikukuu za kipuuzi eti ili kufurahi mwagianeni maji walivyoona tumekubali wakatuletea mfumo wa matope ili tuzidi kuingiza matope zaidi vichwani mwetu hiyo bado haikutosha na sisi kwa fikra zetu zilizojaa matope tukaamua tumwagiane hadi oil chafu bila kujali athari zake nadhani mpango ujao tutapakana vinyesi kabisa by the way you have to be ready fools the plan is coming soon.
Kula keki tu haikutosha katika hayo masikukuu yetu yasiyowajumuisha hata wazazi/walezi wetu waliofanya juhudi za kutuleta hapa duniani na kutulea kinyume chake tunawaalika marafiki zetu tuliokutana nao tukiwa na meno 32 na twafanya sherehe mahali paovu na matendo yamchukizayo Mwenyezi Mungu.
Can I ask a question?
kiburi hiki cha uhai tunakitoa wapi? okay tuendelee tulipoishia.
.......tukaona haitoshi na tukaamua kuanza kubandikana keki usoni huku baadhi ya sehemu kama somalia,yemen,congo,afrika ya kati,sudan n.k kuna watu wakiwemo wazee,wanawake na watoto wanakufa na njaa.
Jamii yetu imekuwa ikiguswa sana na kupiga makelele juu ya maswahibu yanayokuwa yanawakumba watu maarufu kuliko kuweka juhudi katika kuzipigania familia zetu zitoke katika tabaka lililopo hivi sasa yaani tuliurithi ujinga,tunauishi ujinga,tunauendekeza ujinga na kuvirithisha vizazi vyetu ujinga pia
Hivi yule Tanasha wa diamond anatuingizia shilingi ngapi tunavyomnanga mitandaoni eti nyuma kapigwa pasi niulize hivi kwani mlitaka apigwe nini? passport?
Haya leo diamond na Rayvanny kafungiwa kwani wewe mbona umejifungia mafanikio yako na baraza la ujinga na wala hupigi kelele wala kukata rufaa kwa kuyafuata maarifa?
Darassa alikuwa anakula madawa ya kulevya na amerudi akiwa hana hata dalili ya uteja ndani yake vipi unajisikiaje mwafrika mwenzangu hivi ilikulipa nayo hii?
#BringBackOurMo  yeah alirudi and then? mana sisi tulimuita OurMo sijawahi kumsikia akituita My everythingTanzanians.
Tunasifika kwa ukarimu sikatai
Na tukumbuke tunasifika kwa unafiki na uvivu pia upo?
#2019TUACHEUJINGA

Mpango wa manguruwe nyie mnawaita wahisani au wazungu I don't know what the hell are they.
Sio tu kuwafanya mpungue bali na wachache mnaosalia muwe wajinga ukiisoma na kuichimba vizuri historia ya mtu mweusi hutokaa kujikenusha ukimuona mzungu au kujitia mwema mbele ya hawa watu weupe kwa ujumla mana hata wachina,wahindi,na waarabu ni washenzi pia vilevile.
Kati ya watu wenye akili ulimwenguni basi mtu mweusi anastahili kuwa nambari moja kabla ya warusi na waisrael.
Je unaijua historia ya Saa ilianzia wapi? Afrika(Misri) Je Mansa Mussa alikuwa anatokea wapi vile? Afrika(Mali).
Kwani nassa walivyokuwa wanataka kurusha chombo chao kwa mara ya kwanza mwezini walikuwa wanafeli wapi mpaka kikawa kinafeli? unajua ni nani aliyekuja kukiwezesha kiruke? ni yule mama mweusi waliyekuwa wanambagua kisa ana asili ya afrika.
Hivi unamjua Christopher Columbus kweli? Je wakina Martin Luther,Malcom X,Mandela,Nyerere n.k
Je unahitaji reference zaidi? learn to use your brain strictly my friend.

Mitandao ya kijamii naitafsiri kama blanket nzito kutokana na namna akili za vijana wengi kuwa za mfanano na zenye kugubikwa na fikra mgando kutokana na kufurahia maisha fake ya ulimwengu wa nne.
Blanket hili limetupelekea kujiona hatuwezi kuyaendesha maisha kwa usahihi bila ya uongo uongo ndani yake.
Blanket hili limetufanya kuwa wavivu na watumwa kila kukicha.

Kama umelala na hauamshwi kuiona dunia inavyokwenda kasi basi nimeamua kukuamsha kwa kukupa kahawa lita mbili,energy katoni moja na njaa isiyokoma ili usilale tena.
Ila ni maamuzi yako pia kuishi katika ulimwengu wa tatu kwa fikra za ulimwengu wa nne.

BY THE WAY NIWASHUKURUNI SANA KWA KUWA SEHEMU YA KUELIMIKA NA MAARIFA HAYA MUNGU AWABARIKI SANA NA MUWE NA SIKU NJEMA.