Alhamisi, 15 Novemba 2018

USIOGOPE KUSHINDWA

USIOGOPE KUSHINDWA....
Ni kweli kwamba katika kuimarisha kitu chochote kile huchukua muda mrefu sana mpaka kukamilika lakini sio katika kusambaratika kwa kitu hicho huweza kuchukua sekunde,dakika mpaka masaa tu kuporomoshwa kwa ngome iliyojengwa kwa miaka zaidi ya kumi au karne nzima.

KATIKA MAPENZI
Katika ukurasa huu watu wengi tumekuwa ni watumwa wa mateso na uraibu wa athari mbalimbali kutokana na maumivu tuliyowahi kukutana nayo katika kipindi cha kupenda ama kupendwa.
Maumivu yetu yamekuwa siyo ya kukoma kwasababu tumekuwa tukiwakabidhi matabibu watutibu vidonda walivyovisababisha wao wenyewe tukiamini wanajua ni wapi walipolichipua tatizo ili waanzie huko kulitibu na mwisho tumejikuta tukipanua ukubwa na vidonda vyetu kutokana na kuendeshwa na tamaa zetu na wala siyo fikra yakinifu ndani ya vichwa vyetu.
Upo na mtu na unaendelea kuyavumilia mateso na maumivu anayokusababishia au aidha unarudia rudia kufanya kosa lile lile kutokana na kuogopa kuonekana umeshindwa.
Kushindwa siyo kushindikana na kushindikana siyo kushindwa ila moja kati ya hilo linaweza likapelekea ukawa mtumwa wa mateso milele na milele.

TUJIFUNZE KUPITIA MWANARIADHA DEREK ANTHONY REDMOND.
Derek Redmond alikuwa ni mwanariadha mashuhuri kutokea uingereza huko katika karne ya 20.Mnamo mwaka 1992 nchini hispania huko katika jiji la barcelona kwenye mashindano ya olympic huku katika upande wa riadha DereK aliliwakilisha taifa lake la uingereza kama kawaida katika mbio za mita 400. Shindano lilianza vizuri bila ya hitilafu yoyot.
Derek alipofikia mita 100.5 akiwa wa nne kati ya washiriki 10 ghafla nyama za msuli katika paja zilimshika na kumfanya ashindwe kuendelea kukimbia na akaanguka chini huku akiwa anapewa huduma ya kwanza aliinuka na kuanza kukimbia tena kwa kuchechemea na wakati akiendelea kukimbia kwa shida shida mtu mmoja alionekana kuruka wigo kutokea kwenye jukwaa la mashabiki na kuingia katika mzunguko wa kukimbilia kwenye njia  aliyokuwepo Derek na akamfuata ubavuni na kumpa msaada wa egemeo katika upande wa kushoto wa bega la Derek hakuna aliyetambua yule shabiki alikuwa ni nani na walipokaribia kufika katika hitimisho ya mbio zake shabiki yule alimuachilia derek na derek akamaliza mzunguko wake ni kitendo kilichopelekea uwanja mzima kuzizima na kisha kuja kulipuka kwa shangwe sio kwa ajili ya mshindi wa mbio zile bali ni kwa moyo wa kutoogopa kushindwa wa Derek katika tuzo za olympic derek alipata medal ya dhahabu kutokana na kitendo chake cha kutokata tamaa alichokionesha mbele ya hadhara na alipoulizwa je alimtambua shabiki yule aliyemsaidia? derek alijibu ndio yule alikuwa ni baba yangu.
Derek alishindwa kuwa mshindi lakini aliibuka kuwa shujaa wa muda wote katika historia ya riadha kwenye olympic mpaka kesho.

KATIKA MASUALA YA MAISHA NA UCHUMI
Donald trump alishindwa na hata kufilisika mara 11 katika ulimwengu wa uchumi na hata kupelekea kuporomoka katika chati ya ubilionea mara kadha wa kadha lakini hakuwahi kuogopa kushindwa bali alikuwa akikubaliana na hali halisi na mpaka kuwa mkomavu. Erick J. Shigongo wa Global Publishers wakati huu tusingemjua kabisa kutokana na kutaka kujiua kama alivyofanya bilionea wa zamani wa ujerumani aliyejirusha mbele ya garimoshi(treni) kutokana na utajiri wake kupukutika na yeye kufilisika kabisa  huyu aliitwa Mr.Adolf Merckle. Lakini Shigongo zoezi lake halikufanikiwa kutokana na watu wake wa karibu kufanya juhudi za kumuokoa kutoka katika ombwe na jinamizi hilo la kujiua hii ni baada ya kudhulumika Tshs Mil.400 alizokuwa ametaka kuwekeza katika ujenzi wa kivuko huko mkoani Mwanza ziwa victoria.
Lakini pia kumbuka yule aliyekuwa mfalme wa mchezo wa golf hapo kipindi cha nyuma maarufu kama Tiger Wood kuna kipindi aliporomoka kabisa na wengi tulifikiri huyu jamaa labda amestaafu kimyakimya au anauguza majeraha kama mkongwe Michael Schumacher wa formula 1, kutokana na dunia kumpotezea kwasababu ya kufilisika na kugubikwa na skendo na kashfa kadhaa zilizomchafua sana na hali hii ilimpelekea kufikiria kujiua lakini ikafika wakati akaacha kuogopa kushindwa na kweli akashindwa kabisa na miaka ya hivi karibuni akarejea katika hali mpya na akawa bora tena katika ulimwengu wa golf tena kwa kuzirejea nafasi zake zilezile za juu.

katika kitabu kimoja cha Robert T.Kiyosaki maarufu sana cha RICH DAD POOR DAD katika sura ya 7 kuanzia ukurasa wa 164 Robby anaelezea namna ambavyo unaweza kukubaliana na tatizo bila kuathiriwa nalo kwa kutumia falsafa ya watu wa Texas ambao hupenda kusema "when texans win,they win big. And when they lose,it's spectacular." kwa kiswahili maana yake iko hivi "mtexas anaposhinda basi hushinda kwa ukubwa.Na anaposhindwa huvutia."
Kwanini hawa jamaa jambo la kushindwa wanalichukulia ni la kuvutia? Ni kwa kwasababu huwa wanachukulia kushindwa kokote ni sehemu ya hamasa na siyo majuto katika ukurasa wa 167 unwaongelea hivi watexas "They took a great failure and turned it into inspiration" hapo ikiwa inamaanisha kwamba "Huwa wanachukulia kushindwa sana ni sehemu ya hamasa."
Huku naye Robert Kiyosaki katika ukurasa wa 166 amesema hivi "So for most people,the reason they don't win financially is because the pain of losing money is far greater than the joy of being rich." hapa tupafafanue kidogo Uncle Robby alikuwa anamaanisha nini?
alikuwa anamaanisha kwamba kwa watu wengi sababu inayowafanya wasifanikiwe kifedha ni kutokana na maumivu ya kupoteza fedha ni makubwa kuliko furaha ya kuwa tajiri."

TUJIFUNZE KWA WALIOKUWA MABILIONEA NA WAKAANGUKA.
Kila siku inawezekana ukawa unakutana na chati za mabilionea kupanda na kuwa matajiri zaidi duniani kwenye vyanzo mbalimbali vya masuala ya kiuchumi. Lakini ni vigumu kuja kuzipata taarifa za hao hao mabilionea pindi wanapokuwa wameshindwa.
Tunaposema jifunze kwa waliofanikiwa na jifunze kwa walioshindwa pia hatuna maana uende ukajifunze kwa walioshindwa kabisa kuthubutu huwa tunamaanisha ni wale walioshinda kisha wakaja wakashindwa kwani hawa huwa na hadithi zenye mafunzo nyuma yao kuliko wale ambao hawajathubutu kabisa yaani walioridhika na ufukara hawa huwa hawana ushauri wowote isipokuwa lawama na vitisho juu ya jambo unalotaka kulipigania.
Leo kwa ufupi sana nitakuletea orodha ya mabilionea takribani 12 tu ambao walifilisika kwa sababu kuu zifuatazo
1.Kuyumba kwa uchumi ulimwenguni mwaka 2008.
2.Uhaini na ubadhilifu katika masuala ya kifedha.
3.Mikopo (Madeni)
4.Makosa ya jinai
Sasa tuiangazie orodha hiyo

1.EIKE BATISTA bilionea wa kibrazili aliyekuwa anamiliki kampuni za OGX huku akitajwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 30 za kimarekani.Huyu suala la uchumi kuyumba lilimpelekea kukopa na kushindwa kurejesha na baadaye kufilisiwa.

2.BJOGOLFUR GUDMUNDSON bilionea kutokea iceland aliyekuwa kawekeza hisa kubwa katika sekta za kibenki nchini mwake mwake maarufu kama landsbanki inakadiriwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1.1 za kimarekani. Huyu kuyumba kwa uchumi kulimpelekea kuanguka na baadae historia ya ubilionea wake ilibaki katika familia yake kwa mwanae kuendelea kutetea taji hilo mpaka sasa. mwanaye huyu anaitwa THOR BJOGOLFSSON.

3.ALLEN STANFORD  wa Stanford Financial Group aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 8.5 za kimarekani huyu alifilisikia kutokana na uhaini na ubadhilifu wa fedha na anatumikia miaka 110 gerezani tangu mwaka 2009.

4.ELIZABETH HOLMES kutokea Marekani na mmiliki wa Taasisi ya afya iitwayo Theranos ambaye alijipatia utajiri wa dola bilioni 9 za kimarekani kupitia ugunduzi wa njia ya upimaji wa damu kiteknolojia akitajwa kama mwanamke mdogo zaidi kuingia katika orodha ya mabilionea ulimwenguni na kuwa katika orodha ya watu 150 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa mwaka 2015 lakini miaka miwili baadae naye alikuja kufilisiwa kutokana na makosa ya kiuchunguzi yaliyong'amuliwa na maafisa uchunguzi kupitia teknolojia yake kwahiyo faini na kufungiwa kulimpelekea kuanguka.

5.BERNARD MADOFF
Alikuwa maarufu kama mzee wa "ponzi schemes" au split strike conversion ambao ulikuwa ni mfumo wa kifedha aliokuwa ameugundua kwa ajili ya kuwaleta wawekezaji pamoja kuwekeza fedha zao kama amana yenye kupanda na kushuka ilyopolekea taasisi hiyo kuwa na dola bilioni 64.8 za kimarekani na baadae alikuja kuanguka kutokana na kuyumba kwa uchumi mwaka 2008 na mfumo huu wa "ponzi schemes"ndiyo mmoja kati ya uliompelekea ALLEN STANFORD aliyeko namba 4 anayetumikia miaka 110 jela kuingia hatiani kwa kufanya uhaini katika mfumo huu.

6.SEAN QUINN ambaye ni raia wa Ireland aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 6 za kimarekani kupitia kampuni zake za QUINN GROUP ambaye alifilisika kwa kuyumba kwa uchumi,madeni na uhaini wa fedha kupitia makampuni yake ya bima.

7.VIJAY MALLYA ni raia wa kihindi aliyekuwa akiishi nchini uingereza aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya KINGFISHER AIRLINES kampuni aliyokuwa ameirithi akiwa na umri wa miaka 28 na kuifanya  ikue kwa kutengeneza pesa nyingi zaidi kipindi ikiwa mikononi mwake na alikuwa anamiliki utajiri wa dola bilioni 1.5 za kimarekani na alifilisiwa kutokana na mikopo na madeni yaliyokuwa yakimuandama.

8.ADOLF MERCKLE huyu ni bilionea kutokea ujerumani ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa anamiliki utajiri wa dola bilioni 12.8 za kimarekani kupitia kampuni yake ya VEM na alikuja kufilisika kutokana na uchumi kuyumba mwaka 2008 na kumpelekea kushiriki katika kamari alizokuwa kawekea hela kubwa na zikaliwa na baadae mambo yalivyomzidi aliamua kujiua kwa kujirusha mbele ya treni.

9.ALBERTO VILLAR huyu ni raia wa kimarekani aliyekuwa akimiliki kampuni ya AMARANDO INVESTMENT COMPANY na anatajwa kuwa alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1 za kimarekani na alifilisiwa kutokana na ubadhilifu wa kifedha alioufanya  kupitia kampuni yake kwa wanahisa wake na baadaye kutiwa nguvuni yeye na mkurugenzi mwenza wake Mr.TANAKA na wanatumikia kifungo cha miaka 10 jela kutokea mwaka 2005 nadhani watakuwa walishatoka.

10.HUANG WENJI moja ya mabilionea waliokuwa adimu zaidi ulimwenguni kutokana na kujificha sana maana hata picha za huyu jamaa ni za tabu kuzipata. Alikuwa anamiliki kampuni ya CHINA JICHENG HOLDINGS na alikuwa na utajiri wa dola bilioni 1.9 za kimarekani. Alifilisika kutokana na soko la hisa kuporomoka ghafla kwa 91%.

11.PATRICIA KLUGE ni mtarakiwa wa bilionea wa miaka ya 1990 bwana JOHN KLUGE aliyekuwa na utajiri wa dola bilioni 5 na alipata dola milioni 1 baada ya kutarakiana na mumewe ambayo aliielekeza katika biashara zake hasa za rasilimali zisizohamishika (real estates) katika kampuni ya Abramile estate/Kluge estate kwenye upande wa majumba ya kifahari aliyokuwa akiyapangisha na baadaye alifilisiwa kutokana na madeni yaliyokuwa yakimuandana.
Kampuni hii baadae ilikuja kuuzwa na kuchukuliwa na Donald Trump kwa dola milioni 6 za kimarekani.

12.RAMESH CHANDRA ni raia wa india ambaye alikuwa amewekeza zaidi katika sekta ya mali zisizohamishika na alikuwa akimiliki utajiri wa dola bilioni 9.2 za kimarekani katika kampuni yake ya UNITECH REAL ESTATE COMPANY na alikuja kufilisika kutokana na skendo ya mwanae Sanjay Chandra aliyejaribu kudukua mfumo wa mawasiliano serikalini na kutiwa nguvuni mwaka 2011 skendo hii ilimpelekea kulipa mamilioni ya fidia na faini na kumpelekea Ramesh kushindwa kurejesha baadhi ya mikopo katika taasisi za fedha zilizokuwa zikimdai.

KUMBUKA:-Tembo atakonda msimu wa njaa lakini hatorudi kuwa mdogo kama mbuzi, ninavyosema mtu alifilisiwa siyo kwamba ndiyo alirudi chini kabisa na kuwa kama mimi na wewe tunaoogopa kuthubutu au kusonga mbele pindi tunapokabiliwa na nyakati ngumu au tukikutana na majaribu pindi
tukisikiapo hadithi za kusisimua kama hizi kumbuka mabilionea ni wale ambao huanguka na kuinuka mara kadha wa kadha kama alivyoporomoka Yusuph Manji,Donald Trump kutokea nafasi za juu mpakanafasi za mkiani kwa orodha ya forbes ya oktoba mwaka huu.

KUANGUKA KUINUKA KILA MARA ICHUKULIE KAMA MALWEDHE DANCE YA KINGMONADA.
Unajua kuanguka na kuinuka mara kadhaa ni sawa na kucheza nyimbo ya kingmonada ile malwedhe dance yaani unaanguka unaumia na unainuka tena huku ukiwa huna huzuni ya maumivu ya kucheza malwedhe dance basi unakuwa na furaha kutokana na utamu wa nyimbo kwahiyo igeuza hali yoyote ya kuanguka kuinuka katika maisha kama malwedhe dance.
Tambua kuigeuza hali yoyote katika maisha ni kama malwedhe dance kwani hata ule wimbo nao utachezwa sana na kuna wakati utakwisha tu na utakwenda kuimba na kucheza wimbo mwingine katika maisha.

"USIOGOPE KUTHUBUTU KWASABABU UNAOGOPA KUSHINDWA OGOPA KUSHINDWA KABISA KUTHUBUTU"

KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI.
Karibu sana katika darasa maalumu kwa mafunzo maalumu la KNOWLEDGE IS POWER (KIP) ambalo linakwenda kuanza rasmi tar 1/12/2018 kwa msimu huu wa pili litakaloendeshwa kwa siku 14 kwa gharama ya shilingi 7000/= tu.
Thibitisha ushiriki wako kwa hiari kwa kucomment namba yako ya simu ikifuatiwa na neno darasa au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia nambari za simu 0712 335 288 au 0719 342 214.
TUJIFUNZE PAMOJA,TUFANIKIWE PAMOJA.

pia kuna mtazamochanyafoundation group unaloruhusiwa kujiunga bure kabisa ili kupata fikra yakinifu kila siku bonyeza link hapo chini ujiunge moja kwa moja ila hakikisha una nidhamu na unajitambua.

https://chat.whatsapp.com/EM86U47uVzH9aPdGqmMuJJ

#AHSANTENI_WANAMAARIFA_NA_MBARIKIWE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni