MWANAMKE WA WANAWAKE ANAYEWAWAKILISHA AKINA MAMA WOTE ULIMWENGUNI KWA KUWA TAJIRI ZAIDI DUNIANI
Jina lake halisi ni Alice Louise Walton alizaliwa oktoba 7 mwaka elfu tisa mia arobaini na tisa (1949) ni binti wa SAM WALTON ambaye ni mwanzilishi wa WAL-MART STORES INC.
Alice ni raia wa Newport Arkansas Texas marekani katika masomo yake alipita trinity university na kujipatia digrii ya sanaa katika masuala ya fedha na uchumi na baada ya masomo yake hakwenda moja kwa moja kuitumikia kampuni ya familia yake bali alianza kupita katika baadhi ya makampuni kama mfanyakazi kutokana na elimu yake hasa katika mabenki na taasisi nyinginezo za kifedha.
Alice ameolewa na kutarakiana na waume zake mara mbili na hakuna sehemu inayomtaja alice kwamba amewahi kuwa na mtoto/watoto.
Pia alice anatajwa kama mtu mwenye mapenzi makubwa zaidi na sanaa na hata kuanzisha taasisi isiyo ya kiserikali wala faida yenye kujihusisha na masuala kadha wa kadha ya mambo ya kale kama vile taasisi yake iitwayo Amon Carter Museum ya huko nchini kwake Texas.
Nje ya maisha yake pia Alice amekuwa akiandamwa na maswahibu kadhaa ya ajali kwani zimwi hili limemuandana sio chini ya mara moja na kupelekea kufanyiwa upasuaji mara kadhaa.
Alice amekuwa akifuatia nyuma ya mwanamke mwenzake Françoise Bettencourt almaarufu kama (mama wa vipodozi ulimwenguni) ambaye alikuwa nambari 17 akifuatiwa na Alice nambari 18 katika orodha ya Forbes na bloomberg Alice alipanda kuwa mwanamke nambari moja bilionea zaidi duniani baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza kufariki mwaka 2017 mpaka mwezi November mwaka huu(2018) Alice alitajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 47 za kimarekani sawa na trilioni 108 za kitanzania kama sijakosea na anamiliki hisa zenye zaidi ya thamani ya dola bilioni 11 za kimarekani katika kampuni ya familia Walmart stores Inc na hisa hizo ndizo humfanya kuwa kama mrithi mkuu katika kampuni hiyo ya familia.
Hiyo ndiyo historia fupi ya Mama yetu Alice Walton katika MJUE BILIONEA WAKO LEO iliyoletwa kwako na mtazamochanyafoundation billionaire's articles pamoja na udhamini wa Vee's Co.LTD na imeandikwa,kutafsiriwa na kuhaririwa na Mwl.Victor Ramadhan Kalinga.
Ahsanteni na mbarikiwe sana muwe na wiki jema lenye tija na faida mpaka kuisha kwake.
AMINA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni