FALSAFA YA MAISHA (PHILOSOPHY OF LIFE)
(Ph.L)
Kuna ngazi mbalimbali ambazo mwanafunzi hupanda ili kufikia ngazi ya juu ya elimu anayoitaka na kuna ngazi mbalimbali pia ambazo mwanafunzi wa maisha akazitumia aidha kupanda au kushuka ili kufikia kilele cha malengo aliyojiwekea.
Kuitwa dereva,mtumishi,mwalimu,askari,mwandishi,mpishi,daktari,mhandisi, au profesa ni majina ambayo huwa na heshima kubwa kwa mtu na kuitwa mfanyabiashara,mjasiriamali,muwekezaji,mwanzilishi,mgunduzi,tajiri,bosi,bilionea ni majina ambayo huwa na heshima pia.
Lakini katika hayo makundi mawili heshima zake zinatofautiana kulingana na zinavyoundwa au kuandaliwa.
Kuna heshima ambayo tayari imeandaliwa ili uvikwe na kuna heshima ambayo utaiunda na kuiandaa wewe mwenyewe heshima hizi zimetofautiana kwa makundi mawili. Kundi la kwanza ni heshima ya nje na kundi la pili ni heshima ya ndani.
Sitaingia kabisa katika kujadili mifumo ya elimu kwasababu inaweza ikawaathiri wadogo zetu ambao bado wapo mashuleni na vyuoni au wale wote waliotoka kuhitimu hivi karibuni.
Chamsingi cha kuwaambia ni waitegemee elimu kama ngao yao na siyo kama mkombozi wao kwasababu kuna vitu viwili uraiani ambavyo havitangamani kabisa yaani vyeti,mtaa na mihangaiko.
SASA TWENDE TUKASOME UPYA NA TUJITUNUKU Ph.L ZETU BILA JOHO WALA VYETI NA HESHIMA TUKAIPATE VILEVILE.
Watu husema hakuna mwalimu mkorofi,mkali na mgumu kumuelewa kama ulimwengu kutokana na njia anayoitumia kufundisha.
Sijajua ulimwengu ni Madam au Sir ila yeye huanza na kukupatia mitihani mfululizo kisha anakuja kukupatia majibu na baadaye usahihi halafu mitihani tena.
Hapa ndipo wengi hushindwa kumuelewa mwalimu huyu alisomea wapi kufundisha namna hii.
Lakini nilichokipenda kutoka kwa mwalimu huyu tangu nimesajiliwa kwenye darasa lake ni namna anavyowatunuku heshima wanafunzi wake pindi wanapohitimu.
Huwa hatoi cheti,tuzo,medali,kombe wala kitu chochote cha kushikika ila anakuvika vazi la hekima,utu na heshima ambalo siyo la kukodishwa ila huwa anakuja kulinyang'anya ikitokea unalitumia vibaya vazi lake na kukurejesha tena kwenye chumba cha mitihani.
MWALIMU HUTOA SHAHADA YA FALSAFA YA MAISHA YAANI (Ph.L) KATIKA KITIVO CHA MAISHA.
Hekima,utu na heshima utakayovikwa huwa inaambatanishwa na shahada ya (Ph.L) yaani falsafa ya maisha. Na sasa twende tukaiangazie shahada hii kiundani ili uipate unahitaji kupitia katika mitihani ipi.
1.MTIHANI WA KWANZA (CHANGAMOTO)
"Kama ulipo hakuna changamoto basi unaishi mbinguni." ila kama upo kwenye ulimwengu huu huu lazima mtihani huu aidha uliwahi kuufanya ukaishia njiani au kuumaliza au unaendelea kuufanya na bado huelewi idadi ya maswali unayotakiwa kuyajibu hujayajua kwasababu mitihani ya mwalimu huyu hairuhusu kwenda kujibu maswali ya mbele kisha ukaruka ya nyuma ni lazima uyamalize maswali ya nyuma ili ya mbele yawe marahisi.
Mtihani wa changamoto kila mmoja huwa ana wa kwake kutokana na kiwango chake cha kufikiri kwahiyo ukijaribu tu kuigilizia kwa jirani yako utafeli.
Mtihani huu wa changamoto unahitaji hekima wakati wa kuujibu kwani ukienda nao pupa unaweza usiumalize kuujibu. Mtihani huu huja kinadharia na kivitendo kwahiyo utaujibu kwa maandishi na utaujibu kwa vitendo ili kupata usahihi wa majibu uliyoyaandika.
2.MTIHANI WA PILI (NIDHAMU)
Baada ya kutoka katika mtihani wa changamoto unaingia kwenye mtihani wa nidhamu kwani hapa huwa kama kipimo cha majibu ya mtihani wa changamoto.Utahitaji kuujibu kwa nidhamu ya hali ya juu mtihani huu wa nidhamu kwani ndilo daraja la kukuvusha aidha kupanda au kushuka katika kitivo cha maisha.
Utahitaji kuelezea uzoefu wako wa kujiheshimu na kuheshimu wengine,kumuheshimu Mungu na Amri zake,kuheshimu muda wako na wa wengine,kuheshimu fedha unayoipata na unayoitoa kwa kukokotoa thamani na asilimia,faida na hasara,mapato na matumizi,bajeti na akiba,hazina na uwekezaji.
Nadhani ndio maana mtihani huu huwa ni mgumu zaidi kwa wanafunzi wa kitivo hiki kutokana na aina yake ya maswali na ufanyaji kwa ujumla maana hesabu kanuni na njia zake zinazidi zile za albert Einstein,Isaack Newton na wakina archmedes n.k.
3.MTIHANI WA TATU (HEKIMA)
Kama nilivyokuambia hapo awali ili majibu ya maswali ya mbele yawe marahisi hutegemeana na namna utakavyojibu maswali ya nyuma.
Mtihani wa hekima siyo mgumu kama ukifuzu mtihani wa nidhamu kwani maswali yake hufanana na hutegemeana sana.
Kwahiyo hakikisha unakuwa makini na mpole katika kutafuta majibu ya mitihani hii.
Huu ni mtihani ambao utatakiwa kuujibu kihisia zaidi na sauti zilizopo ndani yako kwani huitaji hekima,ustahimilivu na unyenyekevu.
4.MTIHANI WA NNE (SUBIRA)
Unahitaji kuwa na subira sana kuanzia katika mitihani hii kwani mwalimu ambaye ni ulimwengu huwa aidha anachelewesha au kuwaisha majibu kwahiyo hicho nacho huwa ni kipimo na swali katika mtihani huu.
Kuujibu mtihani huu unahitaji kuwa na uzoefu,mifano na kumbukumbu kwani maswali yake hulenga zaidi uhalisia na mapito na namna ulivyojifunza kupitia mapito hayo.
5.MTIHANI WA TANO (UAMINIFU)
Katika chumba cha hii mitihani daima huwa hakuna kusimamiwa na wala muda rasmi wa kumaliza kutokana na kila mtu kuwa na mtihani wake na ukitaka kufeli katika mtihani huu ni pale utakapojaribu kujibu maswali yako kwa majibu ya wengine.
Kuujibu mtihani huu inatakiwa kuwa na hofu ya Mungu kwani ndiye pekee atakayekuongoza kufanya maswali yako kuwa mepesi.
Kwa kipimo maalumu utapimwa na mwalimu ili kuingia katika mtihani huu na kipimo kikikataa wewe kufanya mtihani huu itatakiwa uanze upya kufanya mitihani iliyopita.
Maswali yaliyopo katika mtihani huu siyo yale ya "wiki hii utapokea muujiza mkubwa kama unaamini type amen" usitegemee maswali ya namna hii katika mtihani huu kwani ni mtihani nilioushuhudia watu wakiujibu kwa kulia na kusaga meno.
SASA UNASTAHILI KUVESHWA TAJI NA SHAHADA YA Ph.L KAMA UKIFANIKIWA KUJIBU MITIHANI HIYO.
Huu ndiyo wakati ambao mwanafunzi anakuwa amelegea na kuchoka kabisa na hata wengine kukata tamaa kabisa kwani sherehe ya kutunukiwa kwao huwa siyo ya mbwembwe wala miziki au sherehe ya namna yoyote ile na hakuna ambaye huwa anajua ni lini atahitimu na kutunukiwa shahada yake kwani kila mwanafunzi hufuzu kivyake na kwa wakati wake kwahiyo unatakiwa kuwa tayari kwa majibu yoyote yatakayoletwa na mwalimu huyu kwani hata ukikosea kidogo tu mwalimu hakujumuishi kabisa katika sherehe hii na atakurudisha tena mwanzo katika vyumba vya mitihani.
Pindi mwalimu anapokuletea majibu yako na kukufanyia usahihi huwa hataki kukosolewa,kubishana wala kujibizana kwani mwalimu huyu siyo mbabaishaji wala mwalimu hewa ni mwalimu aliyewafundisha mababu zako,baba zako,na kizazi chako so kuwa mpole usije ukavuruga matokeo dakika za mwisho kisha ukarejeshwa kwenye mitihani japo ni jambo lisilokwepeka ila lisiwe rahisi namna hiyo kutokea kwa kusababishwa na fikra zako mgando.
TUMAINI (FINAL HOPE)
Inawezekana huwaoni wenzako katika chumba cha mitihani hii ukaamini kwamba upo peke yako katika pitio lako na ukachana makaratasi ya majibu yako kwa hofu ya kupata majibu ya kukufedhehesha na kukukatisha tamaa.
Usifanye hivyo kwani ni mapema sana kuchukua maamuzi magumu namna hiyo tupo wengi sana katika chumba hicho kilichogubikwa na giza nene kiasi cha kutoona tunachokijibu ila imani pekee ndio tumaini letu na tunaamini tutatoka salama na kurejeshewa majibu mazuri na mwalimu wetu ulimwengu.
Endelea kufunga na kuomba,endelea kuamini majibu unayoandika ni sahihi,endelea kuamini wewe ndiwe utakuwa mwanafunzi bora pindi majibu yakirejea,endelea kuweka juhudi ya kuandika majibu yako kwa usahihi hata kama mwalimu haangalii mwandiko ye hutazama majibu tu,endelea kuitunza furaha ndogo uliyo nayo hata kama mitihani ni migumu,endelea endelea endelea mbele zaidi usipende kubaki nyuma kirahisi rahisi usikubali kuwekwa kituko na mtumwa na wale waliokwishatunukiwa shahada zao usitamani vya wenye shahada pigania shahada yako kwa hali na mali,jua na mvua,shida na raha,shibe na njaa,milima na mabonde,jangwa na misitu minene,vichaka na mapori pigana.
#MAPINDUZITIME
KARIBU TUJIFUNZE ZAIDI.
Karibu sana katika darasa maalumu kwa mafunzo maalumu la KNOWLEDGE IS POWER (KIP) ambalo linakwenda kuanza rasmi tar 1/12/2018 kwa msimu huu wa pili litakaloendeshwa kwa siku 14 kwa gharama ya shilingi 7000/= tu.
Thibitisha ushiriki wako kwa hiari kwa kucomment namba yako ya simu ikifuatiwa na neno darasa au wasiliana nasi moja kwa moja kupitia nambari za simu 0712 335 288 au 0719 342 214.
TUJIFUNZE PAMOJA,TUFANIKIWE PAMOJA.
pia kuna mtazamochanyafoundation group unaloruhusiwa kujiunga bure kabisa ili kupata fikra yakinifu kila siku bonyeza link hapo chini ujiunge moja kwa moja ila hakikisha una nidhamu na unajitambua.
https://chat.whatsapp.com/EM86U47uVzH9aPdGqmMuJJ
#AHSANTENI_WANAMAARIFA_NA_MBARIKIWE_SANA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni