Jumapili, 23 Juni 2019

MANTA HOFU
Bora ukaogopwa kwa ujasiri wako kuliko uchekwe kwa ujasiri kwasababu ya woga wako.

Msanii Bobby McFerrin katika nyimbo yake ya don't worry be happy katika moja ya shairi lake alisema 
"In every life we have some trouble but when you worry you make it double"
Akiwa anamaanisha 
"Katika kila maisha tuna matatizo fulani na unapoyaogopa ndipo unayazidisha mara mbili."
Kisha akaimba kwa unyenyekevu na utulivu wa kiutu uzima kiitikio chake kisemacho "Don't worry, Be happy." yaani "Usiwe na wasiwasi,kuwa na furaha." 
Kwa kilahaja za kiswahili ni kiarabu,Kingazija na kiunguja twasema MANTA HOFU!

Umri unakimbia hujachumbia,hujaoa/hujaolewa huna mtoto,huna kazi,huna mtaji,huna biashara wala huna elimu.
Rafiki MANTA HOFU kuna Mungu juu aliyetuahidi huwa hawahi wala hachelewi.
Kumbuka Ibrahimu na mkewe Sara walipewa mtoto wakiwa na umri gani?
Ulishawahi kumsikia Kroc,Ford,Sanders wao walipewa ubilionea wakiwa na umri gani vile?

Hivi unakumbuka Mo dewji alivyoshindaga kwa kishindo kula za maoni jimbo la Singida mjini mwaka 2000 halafu akaambiwa we bado mdogo kaa kando kwanza kisha jimbo likaenda kwa mwingine lakini 2005 haikuwa mbali alikuja akachukua kijiti chake maana ilipangwa iwe na kweli ikawa, kwahiyo hata kwako pia unatakiwa kuMANTA HOFU rafiki zamu yako ipo tu.
Samahani rafiki hivi si umeusikia wimbo wa Harmonize Never Give up anasema alikuwa anapenda sana mpira lakini alijaribu na muziki na alivyotua tu BSS wakamwambia hana kipaji hivi angekata tamaa na kurudi tu kusakata kabumbu kwenye ndondo leo tungemjua kweli? Hata wewe Ally Rhymes ndiye unayefuatia mkuu kwahiyo MANTA HOFU juu ya fungu lako zamu yako ipo umaarufu wako upo.
Kumbuka Shigongo aliwahi kupoteza mil.400 bei ya Zhongtong moja new model mpya kabisa mpaka na chenji ya Toyota Allex mbili inarud kwa ajili tu ya kutengeneza kivuko cha kutumika Ziwa Victoria lakini mpaka leo hakijakamilika mkandarasi alimdhulumu Bw.Erick alitamani hadi kujiua lakini baadae AliMANTA HOFU na maisha yakaendelea.
Ukiingia kwenye tovuti ya Forbes utakutana na orodha ya mabilionea 10 waliofirisika kabisa kipindi kile uchumi ulipoyumba wengi walipanic,maana kuna wanaotumikia vifungo virefu jela na wengine walijiua lakini Trump alitakiwa awe miongoni mwao ila aliMANTA HOFU leo huyu hapa!.
Hivi kipindi kile mabasi hayalipi unajua Sumry alipaki yote 80,Ilasi naye alipaki na Ottawa wa songea nae alipaki yote kwa ajili ya kuMANTA HOFU tu hawataki presha hawa jamaa hata kidogo ila leo Ilasi huyu hapa karudi,Sumry yule kule shambani na Ottawa anakomaa na vituo vyake vya mafuta naye kuna fununu atarudi siku sio nyingi.
Sasa wewe una mpenzi tu yaani hata ofisi huna lakini unaumizwa,unanyanyaswa, unachunwa, unasemwa mpaka unakonda mkuu halafu hutaki kuMANTA HOFU kisha ufanye mambo mengine.Onhoo! kama hutaMANTA muda huu ukiwa kijana basi jua mbeleni shida ndio zitakuMANTA.

Hivi unajua Emmanuel Elibariki almaarufu kama NEY WA MITEGO aliunguliwa na chumba alimokuwa anaishi kile kipindi cha Hellouw My love na kupoteza kila kitu pamoja na kuziliwa kale katoto kake kasuriama, unajua alifanyaje? aliMANTA HOFU akakaa sana Iringa pale baadae akarudi upya ndio huyo mpaka leo.
Jifunze kwamba kuna wakati utapoteza kila kitu ili kupata vitu zaidi.

Nakusisitiza sana mkuu/mheshimiwa/mwanamaarifa na rafiki yangu wa kweli kwamba hata iweje hata yaweje MANTA HOFU kama ni kipindi kigumu basi kitapita kama ni matatizo basi yatakwisha na kama ni changamoto jua ndio zinakukomaza na kukuandaa shujaa jasiri na mwenye nguvu pindi ukija kulitwaa kombe lako.
Jiamini
Jikubali
Jifunze
Jitunze
Jipende
Jipe moyo
Jitume
Jithamini
Jitahidi
Jimudu
Jipendelee.


UNGANA NASI
Karibu katika mtazamochanyafoundationgroup tujifunze zaidi bila ya gharama yoyote kwa kubonyeza link hii tiketi yako ni nidhamu,kujitambua na kupenda mabadiliko

AHSANTE SANA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni