Jumapili, 23 Juni 2019

Shule nyingi zipo mjini,ila kuwa makini sana ukiambiwa mjini shule.

Mjini kuna mengi ninayojifunza kila siku tangu nitoke mufindi nyororo kisada ndanindani kule na nikajua kumbe mjini kuna:-
Kutafuta riziki
Kutafuta maisha
Kubangaiza.


Wengi tulioingia mjini kwa lengo kuu la kutafuta maisha tumebaki kuwa wabangaizaji na watafuta riziki mpaka tunapoteza maisha sasa tujitathmini upya na mapema sisi ambao tunaelekea kupoteza maisha na bado tumekomalia ubangaizaji.
Maana kama hatukukosea kuisoma vema kanuni basi tulijibu bila kusoma swali la mwalimu Kashindi Edson lile lisemalo ulikuja kufanya nini hapa duniani?

Mjini kuna wenye mipango ya kutafuta hela,kuna wanaotafuta hela ya malengo na kuna wanaotafuta hela kwa ajili ya pango,jiangalie sana usije ukajichanganya na kutumbukia katika tundu la simba angali wewe ni nyumbu.
Mjini kuna njia za waenda kwa miguu na barabara kuu sasa ikiwa utaendelea kufurahia taa za kwenye njia za waenda kwa miguu ukiamini kwamba serikali inawathamini raia wake kumbuka kamwe hutokuja kutumia kodi yako iliyotumika kujenga na kuimarisha lami ili wewe uje utembelee chombo cha moto.
Mjini kila mmoja kivyake ndio maana muda wa kula ukifika kila mmoja humuoni alipoingilia maana ni tofauti kabisa na atakapokuja kutokea, sawa na safari ya mafanikio tu huyu atawahi na huyu atachelewa hiyo yote ni kutokana na mtu alipoingilia.
Mjini kuna wenye suti na ni smart na kuna wenye akili smart na hawana suti ila nao smart vilevile.

Mjini kuna wadada na wasichana,kuna masister na watawa pia wapo akina mama na wanawake hawa wote ukitumia nguvu kuishi nao utapoteza kila kitu pamoja na nguvu zenyewe.
Mijini kuna biashara na kuna bihasara uchaguzi ni wako aidha ufungue ofisi utengeneze hela au ufungue kijiwe ukashinde kila siku.

Mjini ni mwiko kumuuliza mtu kapata wapi pesa lakini inaruhusiwa kujifunza na kuuliza namna ya kupata pesa.
Mjini bilioni zipo mifukoni mwa watu ila kama za mfukoni mwako zikikushinda kutunza ili zivute za nje basi jua bilioni za nje ndio zinavuta elfu zako.

Mjini sihami maana kila kitu ni rahisi sana kwani ukichoka kulala peke yako unaruhusiwa kulala njaa na usipofanya kazi unakula jeuri yako huku ukishiba faida jua kabisa umekula hasara.
Mjini msiba fursa,kuoa fursa,harusi fursa,kesi fursa,maradhi fursa,ujinga fursa,umalaya fursa,uhuni fursa,taka fursa,sifa fursa,kiki fursa, yaani kila kitu ni fursa ila akili ni ghali zaidi ya ujinga ndio maana mtaji umekuwa changamoto kuu kwa vijana kuchukua fursa.

Mjini kuna Mengi yaani Mo kwa kiingereza ila bado ni mtiti kumpiku Bakharesa.
Mjini kila mtu ni tajiri na ana kila kitu ila tu vyote anavimiliki ndotoni ndio maana akianza kuota anaishia kuvipiga picha na kupost instagram kisha yeye kubaki fukara kwa kukosa usafiri na vibali vya kuhamishia katika maisha halisi.

Mjini kosa kubwa ni kumuamini mtu kwani watu wamezidi kuwa wachache zama hizi na viatu ni vingi kwahiyo chunga sana usije ukavaa cha kukuvaa kisha ukaupoteza utu.
Mjini kila mmoja ni CIA ndio maana kila taarifa wanazo kwahiyo ukija hakikisha hasira zako umeziacha nyingi ulipotoka na huku umekuja nazo hasira chache za kutafutia maisha tu ili usije ukapanic wakati wa kurelax.

Mjini kichwa usibebe kama pambo 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni