NGOME
hakuna anayekomaa na kutarajia kuwa gome bali katika kuwa ngome ugome hutokea.
Inabidi ukae mbali na maji na moto kipindi unajikaza kisabuni kwani maji yatakuacha povu na moto utakuyeyusha.
Maisha yanaweza kukufanya kuwa gome katika safari ya kupigania kuwa ngome.
Kuwa ngome ili kuacha alama ni lazima ukumbane na watu wengi wanaotaka ubaki kuwa gome, yaani wakikuhitaji kama kuni wanakubandua na kukukoka kisha ubaki majivu na wakutupe na wakikuhitaji kama chambo watakukatakata na kukuacha vipande vipande uwakiwe na jua ukauke na ukatike zaidi.
Ngome inajengwa taratibu kwa weredi na kwa ustadi maana ngome ikisimama daima huwa hairudi chini.
Watu wengi wamekuwa magome kwasababu ya kukata tamaa mapema kwasababu ya ngome zao walizokuwa wanazijenga kuyumbishwa na maoni au ufundi mbovu wa mikono yao au mikono ya mafundi waliojinadi ni mahodari na mwisho wa siku wakaleta nyufa katika ngome yako.
Ngome ikisimama husimama daima na huwa haiyumbishwi na upepo au dhoruba jifunze katika ngome ya Yesu kule mombasa.
NGOME NI
Ngome daima ni ngome yaani
Ngome ni msimamo ndani ya nafsi yako
Ngome ni imani na ngao katika maisha yako.
Ngome ni udadisi,kuongeza ujuzi na maarifa.
Ngome ni uthubutu na kuutenga uoga.
Ngome ni kusimamia unachokiona miaka kadhaa mbele hata kama hali ya sasa haikuoneshi matumaini yoyote.
Ngome ni kinara na mfano wa kuigwa kwa jamii yako.
Ngome ni kuishi ndani ya mfumo salama,amri za Mungu,hofu ya Mungu,Maandiko na kuwa kioo cha jamii kwa jamii yako.
Ngome ni kuwa nuru kwa waliopo gizani.
Ngome ni kuwa mfano wa kuigwa na mshiriki wa ujenzi wa maadili mema kwa kizazi chako.
Ngome ni kutetea, kukemea, na kusihi panapobidi.
Ngome ni yule twende na sio tanguliane mimi nakuja.
Ngome ni yule aliyejengwa kwa mwamba chini daima yupo imara hata kama juu watamuona dhaifu.
Ngome ni mjanja kwasababu anajua nini afanye na kuijenga heshima.
Ngome ni msafi wa mwili na msafi zaidi wa akili kuliko wa mavazi ngome sio kuvaa kwa ajili ya kuwatega wakina joel au wasafi wakina joel wapendeze wawanase wakina lili kisha waambukizane upungufu wa akili.
Ngome ni Jambia la maarifa likizungushwa linaizungusha dunia na likiachiwa linaachia maarifa kwa dunia.
NGOME SIO
Ngome sio mchizi boti wa kuniomba hela kipindi nikiwa fukara kisha nikimnyima adai nina roho ya kutu na hila.
Ngome sio mchizi boti anayenipa hela kila wakati ninapomuomba hela, ngome ananipa njia ya kupata hela ili niwe nayo siku nikiwa sina hela.
Ngome sio yule aliyekujua ukiwa na meno thelathini na mawili halafu anakuita damu yako na ukitoka anauza siri zako, ngome ni Baba na mama au walezi wako wanaoyajua madhaifu yako na bado wapo juu yako kukutetea.
Ngome sio yule mpenzi wako aliyekugeuza mgodi kisha moyo akauacha na mashimo ngome ni yule aliyekuja kufukia mashimo na bado hajali hali yako yeye kasimama imara daima kwa ajili yako.
Ngome sio mropokaji lakini ni msemaji mwenye hekima na akisema anasema kilicho wima.
Ngome sio yule anayeandika upuuzi kila anavyojisikia ngome ni yule akiandika anaandikia kwa mataifa na maarifa yanawainua.
Ngome sio yule anayeamini katimia kwa kila eneo na kujitapa,ngome ni yule anayejua kila siku anaamka mjinga na analala mwerevu kwa kila alichojifunza siku nzima.
Ngome sio yule anayeigawa jamii kwasababu ya udini,ubepari,ubinafsi,wivu,jina,rangi,wadhifa,imani,maarifa,elimu nk ngome daima anaupigania usawa.
Ngome sio teja,mlevi,mzinzi,mlafi,mchoyo,mwizi,mjinga na muuaji ngome ni kuijua kweli,kuiishi na kuieneza kwa kila mmoja ili dunia iwe sehemu salama.
Ngome sio yule aliye na sifa zote nilizoziorodhesha hapo juu lakini kila siku anajitahidi kuufikia usafi na kujipendekeza kwa Mwenyezi Mungu.
Mimi ni ngome,wewe ni ngome sisi sote tukiungana tunaweza kuijenga ngome imara lakini kwakuwa tumeambatana na magome na mang'ombe ndio maana tunabaki kuendelea kuonekana mafala.
Ungana nasi bure kabisa ili kujipatia maarifa ya kila siku kwa kuzingatia nidhamu na hekima tu kupitia group letu la whatsApp kwa kugusa link hapo chini.
KARIBU SANA

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni