Jumapili, 23 Juni 2019

ULIMI
Ni heri ya ule ulimi wa mtoto anaoupeleka juu ili kulamba chumvi ya kamasi,kuliko ulimi wa kijana unaoshuka chini kulamba chumvi ya mgodini.
USINIULIZE TUNAKWAMA WAPI?


Ulimi mchafu hauwezi yanena mema ya maendeleo hata siku moja,ulimi mchafu hunena mabaya na kueneza chuki, ulimi mchafu huongeza chumvi katika kila neno kutokana na kuwa na chumvi chumvi nyingi za uchafu za mwili na akili.
Ulimi huleta ufukara ukiendekezwa kuwa huru kutoka kila utakapo na hasa katika kuropoka,kubwabwaja,kubishana,kutusi,kukaripa,kusengenya,kufoka,kulaghai,kudharau na kukejeli.
Ulimi huleta ufukara ikiwa kila umuonapo binti unataka kusema jambo la ushawishi ili kungonoka tambua daima uwekezaji wa chini chumvini hauwezi kukuweka juu labda juu ya kitanda ili kukufikisha kileleni.
Lakini kwa matumizi sahihi ya ulimi ndio yatakupelekea kuanza uwekezaji wa kuanzia chini katika uthubutu wako na ndio utakaokupelekea kuwa juu katika kilele halisi cha mafanikio.
Ulimi haukatai kulambishwa Rizla na jana tulikubaliana itakuwa mwisho wa kuvuta bangi,Ulimi kila pafu unapokea na nikianza kuleta fujo ulimi unajificha, ulimi hutaki niache sigara na pombe kisa unanilaghai ndio starehe zangu huku majuto yangu uzeeni.

Ulimi hauna mfupa na unavunja ndoa.
Ulimi hauna miguu na unaeneza chuki.
Ulimi hauna mamlaka na unawadharirisha wenye mamlaka kuongea pumba.
Ulimi haushiki bunduki na unaua.
Ulimi haujui kujiunga lakini bado unaleta tafrani mitandaoni.
Ulimi hulimi na bado unakula vya mjini
Ulimi hauna vyeti wala shahada na bado unawalaghai wasomi.
Ulimi hausimami lakini unatusimamisha wanaume
Ulimi unakopa na marejesho unakususia.
Ulimi unakiponza kichwa na kujificha tayani.


Ulimi wa fukara ukinena ya busara ulimi wa mwenye hadhi hupinga na kuziita roporopo.
Ulimi wa muhuni hata ukiwa unanena mema unaonekana hauna hoja kwasababu kila baada ya neno ni tusi na kila baada ya tusi ni neno.
Ulimi wa dalali na mfanyabiashara ndio ofisi yake na utupu wa kichwa chako ndio faida yao.
Ulimi wa malaya ni sumu ya akiba na malengo yako.
Ulimi wa baharia ni hatari kwa kijana mpenda vya bure..


HATUJAPOTEZA MUDA
Ni lazima tujue kuvikanya na kuvimudu vitu vidogo vidogo ili vikubwa vije vidumu visije vikaponzwa na tabia hatarishi zinazosababishwa na ulimi.
Jua kujizuia,Jua kujifanya mjinga,Ficha werevu mbele ya wajinga ila usiache kujifunza na kuwapa maarifa,Usiache kujifunza ili ufundishe,Usiache kuonya na kukemea yale maovu,usiache kujitenga na hatari ili kuepusha madhara makuu katika maisha yako.
Nena mema na kemea panapobidi,Sisitiza hofu ya Mungu,wakumbushe amri,waambie bado tu safarini na wasijisahau maana dunia ina mwenyewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni